Juni 13, 2025-Dar Es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida amezikutanisha Timu ya Wataalamu wa Kuandaa Mpango wa Pili wa Maboresho ya Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (MKUMBI II) na Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi kwa kikao-kazi cha kubadilishana uzoefu leo Juni 13, 2025 jijini Dar es Salaam.
Akiongea, katika kikao hicho, Dkt. Kida amesema kuwa lengo kuu la kikao hicho ni kujadili namna kuhuisha mbinu za mashauriano na sekta binafsi na kupata mapendekezo yanayohusu changamoto za Kodi na sizizo za kikodi ili kuhakikisha kwamba Tanzania inakuwa na mazingira Bora ya Biashara na Uwekezaji na Mifumo imara ya kikodi.
Aidha, kikao hicho kimehudhuriwa na Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mheshimiwa Balozi Ombeni Sefue na Wajumbe wa Tume hiyo, na Mwenyekiti wa Wataalamu wa MKUMBI II, Prof. Faustine Kamuzora.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...