Na Mwandishi Wetu
AngloGold Ashanti (Geita Gold Mining Limited -GGML) imesema kuwa inajivunia kwa kiasi kikubwa katika kutekeleza takwa la sheria (Local Content) kwa kuwapa fursa zaidi Watanzania katika maeneo mbalimbali ya utendaji kazi wa mgodi huo katika kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya madini.

Akiongea wakati wa Jukwaa la Nne la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini, Meneja Endelevu wa GGML ambao ni miongoni wa wafadhili wakubwa wa jukwaa hilo linalofanyika mkoani Mwanza Bw. Gilbert Mworia amesema kuwa wamekuwa kinara katika utekelezaji wa sheria ya kuwawezesha Watanzania fursa zinazopatikana katika madini ambapo asilimia 98 ya Wafanyakazi wa mgodi huo ni Watanzania.

Ameongeza kuwa katika kuzijengea uwezo kampuni zinazomilikiwa na Watanzania, GGML imekuwa ikifanya manunuzi ya bidhaa za ndani ( Tanzania ) kwa zaidi ya asilimia 86.

Amesema GGML pia imekuwa na utaratibu wa kuhimiza watoa huduma za ndani wanafuata sheria na taratibu zilizopo katika utoaji wao huduma.

Mbali na hilo, Bw. Mworia amesema kuwa GGML imekuwa ikisapoti Zaidi ya biashara 602 zinazomilikiwa na Watanzania na kuzipa fursa ya kutoa huduma katika maeneo mbalimbali ya mgodi huo.

“GGML kwa kiasi kikubwa tumeshiriki katika michakato mbalimbali ya kuwezesha mafunzo kwa Watanzania katika kuhakikisha wanafuata vigezo vinavyotakiwa ili kuwa washindani katika utoaji huduma”, amesema.

Hata hivyo, ametoa ushauri kwa watoa huduma za ndani kuhakikisha wanafuata masharti yanayohitajika katika tenda wanazoziomba ili kuunga mkono azma ya Serikali ya kuendeleza na kuimarisha ushirikishwaji wa Watanzania (Local content) katika sekta ya madini.

Jukwaa hilo la siku tatu linashirikisha wadau mbalimbali yakiwemo makampuni ya madini na watoa huduma kujadili kwa Pamoja mafanikio na kuangalia namna ya kushirikiana ili kuondoa vikwazo vinavyowakabili watoa huduma wazawa katika maeneo mbali.

Akiongea awali wakati wa utambulisho, Mwenyekiti wa Tume ya Madini Dkt. Janeth Lekashingo ameipongeza Serikali kwa kufanya juhudi mbalimbali , ikiwemo kukuza sekta ya madini na kutoa fursa kwa Watanzania kushiriki kikamilifu katika sekta hii muhimu ya ukuaji uchumi hapa nchini.

Jukwaa hili lenye kauli mbiu “ Ongezeko la Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini , Chachu ya Ukuaji wa Uchumi Tanzania “ linategemea kufunguliwa rasmi Juni 17, 2025 na Waziri wa Madini Anthony Mavunde.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...