*Profesa Msambichaka aweka umuhimu wa umeme wa Nyuklia.

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) imesema kuwa katika mikakati ya Serikali ya kutafuta vyanzo vya umeme hivyo Tume imeona chanzo kingine cha umeme wa Nyuklia.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika warsha iliyoandaliwa imeandaliwa na Tume ya Nguvu ya Atomu Tanzanja pamoja Wakala wa Nyuklia Duniani Mwenyekiti wa Bodi wa TAEC Profesa Joseph Msambichaka amesema kuwa ni mkutano ni muhimu kutokana Serikali kwenda kutekeleza mradi huo.

Amesema ya malighafi ya madini Uranium ya k ipo nchini ya kutosha katika Mikoa ya Ruvuma,Singida pamoja na Dodoma ambapo umeme wake utakaozalishwa ni uhakika.

Profesa amesema kuwa Nyuklia imezoeleka katika uzalishaji wa mabobu lakini Teknolojia imekuwa katika kuzalisha umeme ambapo nchi za Misri,Ghana na Kenya zinatumia umeme huo.

Profea Msambichaka amewatoa hofu watanzania juu ya umeme wa Nyuklia hauna matatizo yoyote na ni wa uhakika na salama kwa matumizi.

Amesema hatua ya serikali kuanza kuzalisha umeme ni kuendeleza Rasilimari hapa nchini kwa manufaa ya Taifa.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), Prof. Najat Kassim Mohammed amesema Warsha hiyo imewakusanisha wadau mbalimbali nchini ,wakiwemo wadau wanahusika na Nishati,Mazingira pamoja na sheria .

Amesema mkutano huo ni kujengeana uwezo wa maarifa kuhusu matumizi Salama ya Nyuklia katika uzalishaji wa umeme.

"Sisi tumepewa jukumu la kuzidhibiti mambo ya Nyuklia na ndio maana tumelichukua,na baadae tutakuja na mapendekezo nini kifanyike"

Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifuwa wa Wizara ya Nishati Mhandisi Innocent Luoga amesema hatua ya kuanza kuzalisha umeme wa Nyuklia imetokana na maelekezo ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Dkt Rais Samia Suluhu Hassan ya kuwataka kuanza kuzalisha umeme Nyuklia pamoja kwenye matumizi mengine.

"Tunazo Rasilimali za Nyuklia ya kutokosha hapa nchini ikiwemo tani 58 0000 maeneo ya Ruvuma,Bayi mkoani Dodoma pamoja na Singida,maelekezo ya Rais yanatupa nguvu "Amesema Mhandisi Luoga.

Hata hivyo,Mhandisi Luoga,amesema sera ya nisharti nchini inataka kuzalisha umeme kupitia vyanzo mbalimbali ili kuwepo na umeme wa kutosha nchini.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) Prof.Joseph Msambichaka akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kuzindua Warsha ya kujadili kuhusiana na Umeme wa Chanzo cha Nyuklia iliyoandaliwa na TAEC pamoja Wakala wa Nyuklia Duniani  iliyoafanyika jijini  Dar es Salaam.
Kamishina wa Umeme na Nishati Jadidifu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Innocent Luoga akizungumza kuhusiana chanzo cha umeme wa Nyuklia na faida zake katika  Warsha ya kujadili kuhusiana na Umeme wa Chanzo cha Nyuklia iliyoandaliwa na TAEC pamoja Wakala wa Nyuklia Duniani  iliyoafanyika jijini  Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) Prof.Najat Kassim Mohamed akizungumza  kuhusiana na umuhimu wa Warsha ya kujadili kuhusu kuwa na chanzo cha umeme wa Nyukilia kwa kuanza kushirikisha wadau pamoja na nchi ambazo zinatumia umeme wa Nyuklia warsha hiyo imeandaliwa na TAEC pamoja Wakala wa Nyuklia Duniani  iliyoafanyika jijini  Dar es Salaam.
Baadhi wadau wakifatilia mjadala kuhusiana na umeme  wa nyuklia jijini Dar es Salaam.


Picha za pamoja za makundi mbalimbali katika warsha ya kujadili umeme nyiklia uliondaliwa na TAEC na Wakala wa Nyuklia Duniani.
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...