NA GATI MSETI,PWANI
KATIKA juhudi za kuongeza uelewa na ushiriki wa vyombo vya habari katika masuala ya usimamizi na uendelezajinwa ardhi nchini,,shirika la Landesa limeanzaa mafunzo maalum Kwa wanahabari kuhusu sera ya ardhi ya mwaka 2023 toleo la 2025.

Mafunzo hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki Kwa siku mbili bagamoyo Mkoani Pwani.

Akizungumza na wanahabari Mtaalam wa masuala ya ardhi kutoka shirika lankinataifa lisilo ka Kiserikali linalojihusisha na masuala ya haki na umiliki wa ardhi(LANDESA)bwn MASALU LUHULA amesema lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwawezesha wanahabari kuelewa mabadiliko yaliyofanywa katika sera hiyo kuelewa athari zake Kwa jamii,na kuwajengea uwezi wa kuriipoti Kwa weledi masuala ya haki ya ardhi,,umiliki na usawa wa kijinsia katika matumizi ya ardhi.

Ameeleza kuwa toleo jipya la Sera lImejikita zaidi katika haki na upatikanaji wa ardhi Kwa makundi maalum kama wanawake ,vijanana jamii za wafugaki sambamba na kushughulikia changamoto za mabadiliko ya tabia nchi na uwekezaji wa kigeni kwenye ardhi.

Awali Kwa niaba ya Mkurugenzi wa Landesa Godfrey Massey ,,Afisa kutoka landesa Queen Mrema amesema kuwa shirika Landesa lilianzishwa 2018 na walijikita katika katika haki za wanawake

Malengo na maeneo waliojikita ni mtumizi Bora ya ardhi,,walijikita katika haki za wanawake ,,uwekezaji ,uharibifu wakihusisha na mabadiliko ya tabia nchi sambamba na kushirikiana na Serikali Katika kufanya mapitio ya Sera na kuishauri Serikali na wadau mbalimbali .

Aidha amesema kuwa wanahabari nisehemu ya sauti Kwa watu ambayo hawasikiki kupitia vyombo vyao vya habari husika na kujenga uelewa Kwa jamii..

Kwa upande wake Mkufunzi wa waandishi wa habari Deotatus Mfugale amesema sera ni muongozo utakaoleta haki usawa kunufaika na rasilimali za nchi sambamba waandishi wa habari kuelewa sera hiyo na kuhoji mamlaka kuhusu muongozo wa sera na utekelezaji wake.

Mwanahabari Hamadi Rashidi amesema kuwa mafunzo hayo yatawasidia wanahabari kuwa sauti ya wananchi katika kushinikiza usawa na uwajibikaji

Sera ya ardhi ya mwaka 2023 toleo la 2025 ni imaboresho ya sera ya ardhi ya wali ya mwaka 1995 na inalenga kuendana na mahitaji ya Sasa ya maendeleo ya taifa,,ukuaji wa idadi ya watu ,,mabadiliko ya tabia nchi nakuongezeka Kwa migogoro ya matumizi ya ardhi nchini Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...