Na Seif Mangwangi, Arusha

MAHAKAMA ya Afrika ya Watu na Haki za Binaadam (AfCPHR), imejiridhisha kwamba inayouwezo na mamlaka ya kusikiliza kesi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo dhidi ya Jamhuri ya Rwanda iliyowasilishwa mahakamani hapo na kutupilia mbali madai ya Rwanda ya kuzuia mahakama hiyo isisikilize kesi hiyo.

Kufuatia kujiridhisha huko, leo Juni 26, 2025 mahakama hiyo imeipatia serikali ya Rwanda siku 90 kujibu madai ya nchi ya DRC na baada ya kuwasilisha utetezi wake mahakamani hapo, mahakama pia itaipatia serikali ya congo siku 45 kujibu majibu ya nchi ya Rwanda dhidi yao na mahakama hiyo itapitia ushahidi wa pande zote na kutoa hukumu.

Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), mwaka 2023 ilifungua kesi dhidi ya Jamhuri ya Rwanda katika mahakama hiyo, ikidai kuwa Rwanda inaunga mkono kundi la waasi la M23, hivyo kuchochea mapigano mashariki mwa DRC.

Aidha DRC inaishutumu Rwanda kwa kuvamia mipaka ya kimamlaka ya Kongo, kuchochea machafuko ya mara kwa mara Mashariki mwa Congo na kusababisha uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo ubakaji kwa watoto, kina Mama , wazee na wagonjwa.

Kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa Februari 12 , 2025 Serikali ya DRC ilikuwa ikiwakilishwa na jopo la wanasheria 18 huku serikali ya Rwanda ikiwakilishwa na mawakili7 ambapo Serikali ya DRC inadai kupitia waasi wa M23, Rwanda inataka kuipindua Serikali halali ya nchi hiyo chini ya Rais Tish2kedi.

DRC inadai kupitia mapigano hayo yaliyoanza mwaka 2021 chini ya ufadhili wa Serikali ya Rwanda na washirika wake yamesababisha watu zaidi ya 500,000 kukimbia makazi yao, huduma za kijamii ikiwemo hospitali na shule kufungwa na kupelekea watoto zaidi ya 20,000 kukosa masomo.

Madai mengine ya Kongo dhidi ya Rwanda yanahusu nchi hiyo kuhifadhi wahalifu wa kivita bila ya kuwachukulia hatua za kisheria au kuwarudisha nchini DRC ili waadhibiwe kisheria.

‎Hata hivyo Rwanda ilikanusha vikali madai ya kushirikiana na makundi ya waasi Nchini DRC ikiwemo kundi la M23 mbele ya mahakama hiyo na kueleza kuwa haina uhusiano wowote na M23 na kwamba Mahakama haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo na kudai inasingiziwa na haina uhusiano na kundi hilo hatari la waasi.

Akisoma uamuzi wa mahakama hiyo leo Juni 26, 2025 Jaji Rafaa Ben Achour wa Mahakama hiyo amesema mahakama hiyo imetupilia mbali maombi ya Serikali ya Rwanda ya kuomba mahakama hiyo ifute shauri hilo lililowasilishwa na Serikali ya DRC kwa kuwa haina mamlaka ya kusikiliza.

‎Hapo awali nchi ya Rwanda ilikataa shauri hilo dhidi ya DRC na kudai kuwa mahakama hiyo haina haki ya kusikiliza shauri hilo kulingana na mkataba wa kuanzishwa kwake .

‎Hata hivyo mahakama imejiridhisha kwamba inayouwezo na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo kulingana na mkataba wa kuanzishwa kwake na hivyo kutupilia mbali maombi ya nchi ya Rwanda .
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...