Mbinga Bila Madiwani: DC Makori Awataka Watumishi Kufanya Kazi kwa Uadilifu.




Mbinga


Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma Kisare Makori,amewataka watumishi Wilayani humo kuhakikisha wanafanya kazi kwa kujituma wakati huu ambao hakuna Madiwani.

Kisare ametoa wito huo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na watumishi na madiwani waliomaliza muda wao wa Halmashauri ya Wilaya Mbinga kwenye sherehe ya kuwaaga madiwani iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.

“nawasisitiza sana umuhimu wa kufanya kazi kwa weledi na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa uadilifu na uaminifu na miradi hiyo ilingane na thamani halisi ya fedha zinazotolewa na Serikali na wadau wengine wa maendeleo”alisema Makori.

Aidha,amewataka kuendelea kuisaidia Serikali kukusanya mapato ya ndani ili kuiwezesha Halmashauri kutekeleza miradi itakayoleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo.

Alisema,Serikali inaridhwa na utendaji kazi wa watumishi wa Halmashauri hiyo kwa namna wanavyofanya kazi kwa kujituma,ushirikiano na weledi hali iliyowezesha kuvuka lengo katika ukusanya mapato ya ndani na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo iliyowezesha kuboresha huduma za kijamii.

Makori,amewapongeza madiwani waliomaliza muda wao kwa kushiriki kikamilifu katika kubuni na kusimamia miradi ya maendeleo na vyanzo vipya vya mapato.

“Mheshimiwa mwenyekiti na Baraza lako mmefanya kazi nzuri sana na nawashukuru kwa ushirikiano mliotupatia ofisi ya Mkuu wa Wilaya,mara kwa mara tulikuwa tunazungumza mambo mengi bila kupingana,ukizungumza jambo watu wako shapu kulifanyia kazi kwa haraka”alisema Makori.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Desdelius Haule,amewashukuru watumishi wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Joseph Kashushura kwa ushirikiano mkubwa waliotoa kwa madiwani katika kipindi chote cha miaka mitano.

Amewakumbusha madiwani waliomaliza muda wao,suala la kuwa wazalendo na kwenda kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza majukumu yake kwa manufaa ya Watanzania badala ya kuwa sehemu ya watu wachache wanaokwamisha juhudi za Serikali ya awamu ya sita.

Haule,amewapongeza waliokuwa wajumbe wa kamati ya fedha uchumi na mipango, kwa kushirikiana na idara ya fedha kuibua vyanzo vipya vya mapato vilivyowezesha Halmashauri hiyo kuendelea kuongoza katika ukusanyaji wa mapato yake ya ndani katika kipindi chote cha miaka mitano.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Joseph Kashushura alisema,madiwani hao wamefanya kazi kubwa ikiwemo suala la ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya ndani kutoka Sh.bilioni 3 wakati wanaingia mwaka 2021/2022 hadi Sh.bilioni 12.2 mwaka 2025.

“nawapongeza kwa kazi nzuri,siyo jambo dogo tangu mmeingia tumekuwa tukisikilizana,hali hiyo imetusaidia Halmashauri yetu kutekeleza miradi mingi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali,tunawashukuru kwa ushirikiano mkubwa mliotupatia kwetu sisi watendaji”alisema Kashushura.

Pia alieleza kuwa,katika kipindi cha miaka mitano Halmashauri imefanikiwa kutoa Sh.bilioni 2.19 kwa vikundi 189 vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu na Sh.bilioni 1.

Amehaidi kutekelezwa na kukamilishwa miradi yote iliyobuniwa kati ya watendaji na madiwani hao ikiwemo mradi wa ujenzi wa jengo la kituo cha uwekezaji kilichopo Mbinga Mjini na ujenzi wa majengo kwenye kituo cha uwekezaji eneo la Mkako.

“nina uhakika mtakaporudi kwa mara nyingine tena baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba mtakuta vitu vingi vimeanza kufanyiwa kazi na vinaendelea kutekelezwa”alisema.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...