NAIBU wa Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis amewataka wananchi wanaofanya shughuli kwenye fukwe kutoharibu mazingira na badala yake wafuate sheria ikiwemo kutotupa taka ovyo.

Ametoa wito huo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Asya Mwadini Mohammed aliyetaka kujua mkakati wa Serikali wa kusimamia utunzaji wa mazingira ya fukwe.

Akiendelea kujibu swali hilo, Naibu Waziri Khamis amesema kuwa Serikali inaendelea kuchkua hatua za kusimamia sheria ambayo inawataka wananchi kuacha kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya mita 6o kando mwa vyanzo vya maji.

”Ni kweli kuna baadhi ya shughuli zinafanyika kwenye kingo za bahari, kingo za mito na hata kingo za mawiwa ambayo ni vyanzo vya maji vinavyosaidia shughuli za kiuchumi na sasa zipo hatua ambazo Serikali tumezichukua ikiwemo usimamizi wa sheria na kutoa elimu,” alisema.

Aidha, Mhe. Khamis alisema Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana Mamlaka ya Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) itaendelea kupambana na vitendo vya uharibifu wa mazingira katika Mlima Kilimanjaro vikiwemo uchomaji wa moto.

Alisema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Shally Raymond aliyetaka kufahamu Serikali ina moango gani wa kuhakikisha theluji ya Mlima Kilimanjaro ambayo ni kivutio cha utalii haiyeyuki.

Mhe. Khamis alisema Serikali itaendelea kutumia sheria, miongozo, kanuni na kampeni ambazo zina maelekezo ya mbalimbali ya utunzaji wa vyanzo uvya maji, upandaji miti, kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Awali, akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Esther Malleko lililoulizwa kwa niaba yake na Mhe. Shally kuhusu Serikali ina mpango gani wa kudhibiti uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli za kibinadamu, Mhe. Khamis alisema uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli za kibinadamu unatokea katika sekta nyingi nchini.

Hivyo, alisema ili kudhibiti uharibifu huo, Serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kuandaa Sera, Sheria kanuni mikakati na miongozo mbalimbali inayobainisha hatua zinazochukuliwa kukabiliana na changamoto hizo.

Alitaja Sera ya Taifa ya Uhifadhi wa Mazingira ya 2021, Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Sura 191 ikisomwa pamoja na marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Na.5/2025 na Mpango Kabambe wa Taifa wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (2022-2032) ni hatua zilizochukuliwa.

Naibu Waziri Khamis aliongeza kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais itaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu uhifadhi wa mazingira na changamoto za mabadiliko ya tabianchi kwa njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari, ziara za viongozi na mafunzo mashuleni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...