NAIBU Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, amepongeza Shirika la Mawakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwa namna linavyotekeleza kwa ufanisi majukumu yake katika kusimamia sekta ya usafiri wa majini nchini.

Mhe. Kihenzile alitoa pongezi hizo alipotembelea banda la TASAC katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2025 yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma. Maonesho hayo yanalenga kuonesha namna taasisi za umma zinavyotekeleza majukumu yao kwa uwazi, uwajibikaji na ufanisi, huku yakitoa fursa kwa wananchi kufahamu huduma zinazotolewa na Serikali.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri alipata maelezo ya kina kutoka kwa Afisa Mkaguzi na Msajili Mkuu wa Vyombo vya Usafiri Majini kutoka TASAC, Bw. Said Mkwawa, ambaye alieleza kuwa majukumu ya msingi ya shirika hilo ni pamoja na kusimamia na kuratibu shughuli zote za uwakala wa meli nchini, kusajili na kukagua vyombo vya usafiri majini, kusimamia usalama na ulinzi wa usafiri wa majini, kutoa mafunzo na usajili wa mabaharia pamoja na kuwezesha utekelezaji wa mikataba ya kimataifa kuhusu usafiri majini.

Bw. Mkwawa alibainisha kuwa TASAC imeendelea kuboresha mifumo yake ya usimamizi na huduma kwa wananchi, kwa lengo la kuhakikisha usafiri wa majini nchini unakuwa salama, wa kuaminika, na unaochangia kikamilifu katika ukuaji wa uchumi wa taifa, hasa katika maeneo ya ukanda wa pwani na maziwa makuu ambako usafiri wa majini ni kiungo muhimu cha maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2025 yanafanyika chini ya kaulimbiu: “Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidijitali Ili Kuongeza Upatikanaji wa Taarifa na Kuchangia Uwajibikaji,” yakiwa yanashirikisha taasisi mbalimbali za serikali kutoka sekta mbalimbali, ambapo TASAC ni miongoni mwa taasisi zilizoonesha mafanikio na maboresho ya huduma zake kwa umma.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mkaguzi na Msajili Mkuu wa Vyombo vya Usafiri Majini kutoka TASAC, Bw. Said Mkwawa kuhusu kazi mbalimbali za Shirika hilo alipotembelea banda la Shirika la Mawakala wa Meli Tanzania (TASAC) wakati wa maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2025 yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma. 
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile akizungumza na watumishi wa TASAC alipotembelea banda la Shirika la Mawakala wa Meli Tanzania (TASAC) wakati wa maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2025 yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma. 
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile akisaini kitabu katika banda la Shirika la Mawakala wa Meli Tanzania (TASAC) wakati wa maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2025 yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma. 
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Mkaguzi na Msajili Mkuu wa Vyombo vya Usafiri Majini kutoka TASAC, Bw. Said Mkwawa kwa niaba ya Shirika la Mawakala wa Meli Tanzania (TASAC) wakati wa maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2025 yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...