Na Mwandishi Wetu
KATIKA Kuadhimisha Siku ya Mazingira duniani, Kampuni ya Oryx Gas imetoa elimu ya usafi wa mazingira pamoja na matumizi bora ya nishati safi ya kupikia katika shule ya msingi Kisiwani iliyopo Kigamboni mkoani Dar es Salaam.
Akizungumza katika Juni 5, 2025 katika zoezi hilo, Meneja Miradi Nishati Safi ya Kupikia wa kampuni hiyo Peter Ndomba amesema kampuni hiyo inaamini elimu ambayo wameitoa kwa wanafunzi hao ya kutumia gesi kwa usalama wataipeleka kwa wazazi wao na kusisitiza wamewaeleza kwanini kuna umuhimu wa kutunza miti.
“Sasa hivi hali ya hewa imebadilika mvua inanyesha tu, huu ni mwezi wa sita lakini mvua bado zinanyesha na sababu hali ya hewa imebadilika kwa nchi nyingi duniani.Hivyo Watanzania tunawajibu kuendelea kutunza mazingira na tunarithisha kwa kizazi hiki cha watoto hawa.
“Lakini tumewapa elimu hii kwa kutambua wakiipata mapema itasaidia kuwa na jamii inayotambua umuhimu wa kutunza mazingira badala ya kuipata elimu hii wakiwa wakubwa.Katika hii siku ya mazingira duniani sisi Oryx kwa kushirikiana na wadau wengine tunawahamsisha wananchi wasiharibu mazingira na kutoharibu mazingira.”
Amefafanua na kutoharibu mazingira ni kuwa na njia mbadala ya kutunza mazingira kama kuwa na nishati safi ya kupikia.Hivyo wanapotoa elimu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia wanalenga kuondoa uharibifu wa mazingira“Kwahiyo tunatumia siku ya leo kuwakumbusha watu mazingira ndio maisha bila mazingira bora hatuna maisha.”
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kisiwani Abbas Degelo ameishukuru kampuni hiyo kwa kuungana na shule hiyo kufanya usafi wa mazingira ya shule hiyo sambamba na kukabidhi vifaa vya kuhifadhia taka.
“Nitoe shukrani nyingi kwa Oryx Gas kwa kutushirikisha katika usafi wa mazingira hivyo kusaidia kutengeneza mazingira ya shule kuwa masafi.Naomba jamii pia itumie nishati safi ya kupikia ambayo ni marafiki wa mazingira lakini gharama ya gesi iko chini ukilinganisha kuni na mkaa.
Wakati huo huo wanafunzi wa Shule ya Msingi Kisiwani wakiongozwa na Dada Mkuu Abigael Baraka na Mwakilishi wa Kaka Mkuu wa shule hiyo Gerevas Yusufu wamesema wanashukuru kwa kupata elimu ya matumizi salama ya nishati safi pamoja na kufanya usafi wa mazingira ambapo wameahidi watakuwa mabalozi wa kufikisha elimu hiyo kwa wengine ili kuwa na jamii yenye mtazamo mmoja katika kutunza mazingira.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...