NA MWANDISHI WETU

Taasisi ya Saratani Ocean Road, imeweka kambi katika viwanja vya Bunge jijini  Dodoma na kutoa huduma za kibingwa na kibobezi za uchunguzi na tiba kwa wagonjwa wa saratani.

Hatua hiyo imefikiwa ikiwa ni wiki ambayo Bajeti ya Wizara ya Afya imewasilishwa na kupitishwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania.

Akizungumza na timu ya wataalamu na madaktari bingwa wa magonwja ya Saratani Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Festo Dugange, amepongeza hatua hiyo na kutoa wito kwa wabunge, watumishi wa Bunge na wageni mbalimbali wanaofika katika maeneo hayo kuitumia fursa hiyo kufanya uchunguzi wa magonjwa ya saratani.

Kwa upande wa Madaktari Bingwa wa kambi hiyo Meneja wa Huduma za Uchunguzi wa  saratani na elimu kwa umma kutoka Ocean Road Dkt. Maguha Stephano, ameahidi taasisi hiyo itaendelea kuhakikisha inaendelea kutoa huduma za kibingwa na kibobezi za saratani kwa wabunge na wananchi.

Alisema, huduma mbalimbali zinatolewa ikiweno za uchunguzi, elimu , ushauri wa saratani na kuendelea kutoa  huduma kupitia mkoba za kibingwa mikoani , huduma hizi maarufu kama Rais Dkt.Samia Suluhu Outreach Services zilianza kutolewa mwaka 2021, lengo likiwa ni kupunguza vifo vitokanavyo na magonjwa ya saratani nchini.

“Katika miaka hii minne ya Rais Dkt. Samia taasisi imeweza kuifikia mikoa 32 na wananchi  78,959 wamefanyiwa uchunguzi wa saratani mbalimbali,”alisema.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...