Serikali itaendelea la kutoa mafunzo ya Mtaala uliboreshwa kwa walimu wote nchini ili kuhakikisha wanakuwa bora katika eneo la ufundishaji na ujifunzaji shuleni huku akiwataka walimu wote waliopata mafunzo ya somo la elimu ya biashara nchi nzima kuwa na mtizamo mpya katika kufundisha somo hilo . 

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Elimu kutoka ofisi ya Rais na Utawala Bora TAMISEMI, Bw. Atupele Mwambene  aliyemwakilisha mgeni rasmi , Katibu TAMISEMI ,Bw. Adolf Nduguru  kwenye ufungaji wa mafunzo ya walimu wa ajira mpya wa somo la Elimu ya Biashara katika mtaala ulioboreshwa leo tarehe 11/6/2025 katika chuo cha Ualimu Korogwe , Mkoani Tanga.

Amewataka kuhakikisha wanakuwa na mtizamo chanya katika kufundisha somo hilo la elim u ya baishara kwa kuhakimisha wanakwenda shuleni kuwafundisha walimu vyema ili waweze baadae kutumia somo hilo katika kujiajiri wenyewe kwa namna watakavyoweza kuwandaa .

“Hakikisheni mnakuwa na mtizamo chanya mnaporejea katika vituo vyenu vya kazi haya mafunzo yakalete mabadiliko kwa wanafunzi nchini kwani maboresho kayika mtaala umewekwa masuala ambayo yatamsaidia  mwanfunzi katika kujifunza vyema suala la biashara” amesema Bw. Mwambene.

Pia ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuboresha elimu nchini ikiwemo kutoa ajira kwa walimu nchini pamoja na kuidhinisha fedha za mafunzo kwa walimu wote nchini na kuendelea kuimarisha sekta ya elimu.

Katika hatua nyingine ameitaka Tassis ya Elimu Tanzania (TET)kuhakikisha inaendelea kuimarisha mafunzo endelevu kazini(MEWAKA) kwa walimu wote ili waweze kuendelea kujifunza katika jumuia za ujifunzaji kuongeza ujuzi na uelewa wa  masomo kazini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba amewaasa walimu hao kuwa chanzo cha mabadiliko katika ufundishaji wao kwa somo hilo la elimu ya biashara  na kusema kuwa mbinu walizojengewa katika mafunzo hayo wazitumie vyema katika kuhakikisha wanakuwa bora.

“Hakikisheni mnazingatia yote mliyofundishwa kwenye mafunzo haya  myatumie vyema mnaporejea katika viruo vyenu vya kazi , naomba sana mzingatie yote mliyofundishwa ili mkalete mabadiliko”amesema, Dkt. Komba

Naye Afisa Elimu wa Korogwe  Bi.Mary Mmari amesema kuwa mafunoz haya yanatija kwa walimu wote walioweza kuyapata hivyo amewaomba walimu hao wawe sehemu ya mabadiliko.

Kwa upande wake mwakilishi wa Shirika lisilo la kiserekali la EDUCATE, Bw. Nelson Musikula amesema, kama wadau wataendelea kutoa ushrikiano katika kuinua elimu nchini hasa katika somo la elimu ya biashara ili kuwezesha wanafunzi wote nchini wanapata uelewa na kuweza kujifunza namna ya kuanzisha biashara.

Jumla ya walimu idadi ya  1913 wamepata mafunzo ambapo katika kituo cha  chuo cha ualimu Tabora jumla ya walimu walikuwa  513, kituo cha chuo cha Morogoro  ni idadi ya  791 huku  Chuo cha Ualimu  Korogwe wakiwa idadi ya  609.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...