Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mohamed Mchengerwa amesema uchaguzi wa wanafunzi wa Kujiunga na Kidato cha tano katika Shule za Sekondari, Vyuo vya Elimu ya Ufundi vya Serikali Mwaka 2024, umekamilika, Uchaguzi huo umefanyika kwa kuzingatia utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2023 na Mtaala ulioboreshwa.
Mchengerwa ameyazungumza hayo Leo jijini Dodoma katika Mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema, Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka Shule za Serikali, zisizo za Serikali na watahiniwa wa kujitegemea waliofanya mtihani chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.
"Jumla ya Watahiniwa walioandikishwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka, 2024 walikuwa ni 529,329 wakiwemo Wasichana 278,771 (52.66%) na Wavulana 250,558 (47.34%). Kati yao Watahiniwa wa Shule waliosajiliwa walikuwa 557,796 wakiwemo Wasichana 296,051 (53.08%) na Wavulana 261,745 (46.92%), Watahiniwa wa Kujitegemea walikuwa 28,467 kati yao wasichana walikuwa 17,280 (60.70) na wavulana 11,187 (39.30)" - Mchengerwa
Aidha, Katika ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja, unaonesha kuwa Watahiniwa 223,372 (41.23%) walipata ufaulu wa Daraja la I III, hali inayoonesha kuwa Ufaulu wa watahiniwa wa mwaka 2024 umeongezeka kwa 5.36% ikilinganishwa na ufaulu wa Daraja la I III wa watahiniwa 198,394 (35.87%) wa mwaka 2023.
Jumla ya wanafunzi 214,141 wakiwemo wasichana 97,517 na wavulana 116,624 walibainika kuwa na sifa za kuchaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi ikijumuisha wanafunzi 1,028 wenye mahitaji maalum kama ifuatavyo:-
Wanafunzi 149,818 sawa na asilimia 69.96 wakiwemo wasichana 76,491 na wavulana 73,327 wenye sifa wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano katika Shule 694 za sekondari za Serikali kama ifuatavyo:-
Wanafunzi 1,728 wakiwemo wasichana 801 na wavulana 927 wamepangwa katika shule za sekondari 08 zinazopokea wanafunzi wenye ufaulu wa juu zaidi,
Wanafunzi 141,146 wakiwemo wasichana 72,337 na wavulana 68,809 walipangwa katika shule za bweni na Wanafunzi 6,944 wakiwemo wasichana 3,353 na wavulana 3,591 wamepangwa katika shule za kutwa.
Wanafunzi 2,875 wakiwemo wasichana 1,057 na wavulana 1,818 wamechaguliwa kujiunga na fani mbalimbali katika Vyuo 04 vya Elimu ya Ufundi, vyuo hivyo ni Chuo cha Ufundi cha Arusha (ATC), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) na Chuo cha Maendeleo ya Maji (WMDI),
Wanafunzi 2,214 wakiwemo wasichana 1,099 na wavulana 1,115 wamechaguliwa kujiunga na Vyuo vya Afya ngazi ya Stashahada,
Wanafunzi 1,609 wakiwemo wasichana 443 na wavulana 1,166 wamechaguliwa kujiunga na Vyuo vya Ualimu kozi za Stashahada na
Wanafunzi 57,625 wakiwemo wasichana 18,427 na wavulana 39,198 wamechaguliwa kujiunga na Vyuo vya Kada mbalimbali.
Mchengerwa amesema muhula wa kwanza kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano utaanza tarehe 08 Julai, 2025. Hivyo Wanafunzi wote waliopangwa kujiunga na Kidato cha Tano kwa mwaka, 2025 wanapaswa kuanza kuripoti Shuleni kuanzia tarehe 06 Julai, 2025. Siku ya mwisho ya kuripoti itakuwa tarehe 21 Julai, 2025.
Kwa wanafunzi waliopangwa kwenye Vyuo vya Elimu ya Ufundi watapokea maelekezo ya namna ya kujiunga kutoka katika Vyuo walivyopangwa.
Uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo umefanyika kwa kuzingatia ufaulu na nafasi zilizopo; hivyo, hakutakuwa na fursa ya kufanya mabadiliko yoyote ya Shule kutokana na ukosefu wa nafasi.
Mchengerwa ametumia nafasi hiyo kuwapongeza walimu, wazazi na walezi wote kwa juhudi walizozifanya katika malezi na ufundishaji hali iliyowezesha wanafunzi kufaulu vizuri.
"Naomba wazazi/walezi wote tuendelee na moyo huu wa kusimamia na kufuatilia maendeleo ya watoto wetu. Aidha, nawapongeza wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi"
Hata hivyo Mchengerwa amewahimiza wanafunzi kuendelea kufanya bidii katika kujifunza ili waweze kufanikiwa kujiunga na mafunzo ya Elimu ya Juu baada ya kuhitimu Kidato cha Sita na Vyuo vya Elimu ya Ufundi.
"Ninawashukuru Viongozi na Watendaji wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, wadau wote wa Elimu, pamoja na Wananchi wote kwa ujumla kwa kushiriki kikamilifu kuimarisha miundombinu ya Shule ikiwemo ujenzi wa madarasa, mabweni na majengo mengine yaliyowezesha shule kupokea wanafunzi wote waliopangwa kujiunga na Kidato cha Tano.
Waziri huyo ametoa wito kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha kuwa azma ya Serikali ya kuwa na Shule za Sekondari za Kidato cha Tano katika kila Tarafa inatekelezwa, ili kuwezesha wanafunzi wote wanaofaulu Mtihani wa Kidato cha Nne kupata nafasi ya kuendelea na masomo ya Kidato cha Tano na Sita, Upanuzi na ujenzi wa Shule Mpya za Kidato cha Tano na Sita uendelee kufanyika ikiwa ni pamoja na kuongeza tahasusi za masomo ya Sayansi. Mikoa ihakikishe inakuwa na tahasusi zote za msingi katika shule zake ili kuwapunguzia wazazi/walezi na wanafunzi gharama za usafiri kwenda shule za mbali.
Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa na Fomu za kujiunga na Kidato cha Tano, Vyuo vya Elimu ya Ufundi mwaka, 2025 inapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Rais -TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz na Baraza la Taifa la Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi www.nactvet.go.tz.
Mwisho Mchengerwa amesema pamoja na maelekezo hayo, kwa mwanafunzi, mzazi/mlezi atakayekuwa na suala linalohitaji maelekezo au ufafanuzi zaidi aende katika Ofisi za Elimu za Mikoa na Halmashauri au apige simu kwenye namba ya Kituo cha huduma kwa wateja cha OR-TAMISEMI kwa namba za simu 026 160210 au 0735 160210 kwa msaada zaidi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...