Na Mwandishi Wetu

Serikali imetoa wito kwa jamii kujenga utamaduni wa kupanda na kutunza miti ya matunda na kivuli ili kuboresha mazingira, hususan katika Jiji la Dodoma na maeneo mengine nchini, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuikijanisha Tanzania.

Wito huo umetolewa hivi karibuni na Afisa Misitu wa Wilaya ya Kondoa, Clement Kabeni, wakati wa zoezi la upandaji miti katika Shule ya Msingi Chungai na Shule ya Sekondari Imbafi, wilayani Kondoa.

Kabeni alisema miti hiyo, iliyotolewa na shirika lisilo la kiserikali la INADES-Formation Tanzania, inapaswa kutunzwa vizuri ili ikue na kuchangia kuboresha mazingira ya shule hizo na jamii inayozunguka.

"Tunaomba sana miti hii itunzwe, iwe inamwagiliwa mara kwa mara ili ikue na kuleta faida kama kivuli na matunda kwa vizazi vijavyo. Zoezi hili ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani," alisema Kabeni.

Aidha, alilishukuru shirika la INADES-Formation Tanzania kwa mchango wao mkubwa katika upandaji wa miti wilayani humo, ambapo hadi sasa zaidi ya miti 37,200 imepandwa katika maeneo mbalimbali ya Kondoa.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa shirika hilo, Mbarwa Kivuyo, mwakilishi wa INADES-Formation Tanzania, Rajabu Rajabu, alisema shirika litaendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha mazingira yanatunzwa kupitia kampeni za upandaji miti ya kivuli na matunda katika vijiji vya Kondoa na maeneo mengine ya Mkoa wa Dodoma.

"Tumeadhimisha Siku ya Mazingira Duniani mwaka huu kwa kupanda miti katika Wilaya za Chemba na Kondoa. Tunawaomba walimu na viongozi wa wilaya kushirikiana kutunza miti hii kwa kuihudumia kila siku," alisema Rajabu.

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chungai, Nasibu Mkorongwe, alisema shule yao imeadhimisha siku hiyo kwa kupanda zaidi ya miti 100 ya matunda na mbao, na kwamba kila mwanafunzi atapewa jukumu la kuitunza mti mmoja hadi utakapo komaa.

"Lengo letu ni kufikia miti 1,000 ifikapo mwaka 2026. Tunawahakikishia INADES kuwa miti hiyo itatunzwa kwa uangalifu mkubwa," alisema Mkorongwe.

Siku ya Mazingira Duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 5 Juni, ambapo kwa mwaka huu maadhimisho kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma, yakihudhuriwa na Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango, ambaye alikuwa mgeni rasmi.John Milton, Afisa Ufwatiliaji na Tathmini, wa Shirika lisilokua la kiserikali la INADES-Formation Tanzania, akishiriki zoezi la upandaji miti ya matunda katika Shule ya Sekondari ya Gwandi, Wilayani Chemba wakati wa madhimisho ya siku ya Mazingira Duniani iliyofanyika  hivi karibuni jijini Dodoma. Shirika la INADES-Formation Tanzania limeadhimisha siku ya Mazingira Duniani kwa kupanda miti mbalimbali katika vijiji vya Wilaya za Chemba na Kondoa mkoani Dodoma.


Mkuu wa Idara ya Mafunzo wa shirika lisilokua la kiserikali la INADES-Formation Tanzania Jacqueline Nicodemus akifurahia jambo alipotembelea banda la shirika hilo wakati wa maadhimisho ya siku ya Mazingira duniani yaliyofanyika kitaifa viwanja vya Jakaya Kikwete jijiini Dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...