SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewahakikishia wananchi kuwa Watanzania walioko nchini Israel na Iran wako salama, licha ya hali tete ya usalama kufuatia mashambulizi yaliyoanza tarehe 13 Juni 2025 kati ya mataifa hayo mawili.

Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Juni 19, 2025 imeeleza kuwa Mashambulizi hayo, ambayo yamesababisha wasiwasi mkubwa kimataifa, yameifanya Tanzania kuanza kuchukua hatua za dharura za kuwaokoa na kuwarejesha nyumbani raia wake walioko katika maeneo yaliyoathirika. 

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Kupitia Balozi zake zilizopo nchini Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu (ambayo inaiwakilisha Tanzania nchini Iran), Kuwait na Israel, Serikali inaendelea na juhudi za kuwaorodhesha Watanzania waliopo katika maeneo hayo ya mgogoro.

"Taarifa za hivi karibuni zinaonesha kuwa kuna Watanzania 168 walioko nchini Iran, wakiwemo wanafunzi 134 katika mji wa Qom na wengine 34 jijini Tehran. Nchini Israel, inakadiriwa kuwa wapo zaidi ya Watanzania 200, wakiwemo watumishi wa Ubalozi wa Tanzania, wanafunzi, na wafanyakazi wa taasisi mbalimbali. Kati yao, Watanzania 50 tayari wamejiandikisha kwa ajili ya kupatiwa msaada wa kurejea nyumbani."

Katika taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imethibitishwa kuwa jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Israel halijaathirika na mashambulizi ya hivi karibuni ya Iran.

Aidha, wakati mashambulizi yalipotokea, hapakuwa na mtu yeyote ndani ya jengo hilo, na maafisa wa ubalozi pamoja na familia zao wote wameripotiwa kuwa salama.

Balozi za Tanzania nchini Israel na Umoja wa Falme za Kiarabu zimekuwa zikiwasiliana moja kwa moja na Watanzania walioko maeneo hayo, zikiwasihi kuchukua tahadhari za kiusalama huku Serikali ikiendelea kushughulikia mipango ya kuwaondoa katika maeneo ya hatari.

Serikali, kwa kushirikiana na wadau wake wa ndani na nje ya nchi, inaendelea na taratibu za kiutendaji kuhakikisha kuwa Watanzania waliopo katika maeneo hayo ya migogoro wanarejeshwa nyumbani salama haraka iwezekanavyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...