SHIRIKA la Masoko ya Kariakoo linawataarifu wafanyabiashara pamoja na wananchi wote wanaohitaji maeneo ya kufanyia biashara katika Soko la Kariakoo kwamba sasa wanaweza kujisajili kwenye mfumo wa kielektroniki wa TAUSI PORTAL ili kushiriki katika mnada wa kupata maeneo hayo.

Kupitia anwani ya www.tausi.tamisemi.go.tz, wafanyabiashara wataweza kuona maeneo yote ya biashara yaliyotangazwa kwa njia ya mnada. Mnada huu wa kielektroniki utafanyika kuanzia tarehe 05 Juni, 2025 saa 1:00 Asubuhi hadi tarehe 11 Juni, 2025 saa 1:00 Asubuhi.

Ili kushiriki, mfanyabiashara anapaswa kujisajili kwenye mfumo wa TAUSI PORTAL akiwa na taarifa zifuatazo:


Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA)

Namba ya Mlipa Kodi (TIN)

Barua pepe (Email)

Namba ya simu

Wananchi na wafanyabiashara wote mnaombwa kutumia fursa hii muhimu kwa ushiriki wa haki na uwazi.

Imetolewa na:
Ashraph Y. Abdulkarim
MENEJA MKUU
Shirika la Masoko ya Kariakoo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...