Suluhisho za Kisasa za SICPA Zinaongeza Imani ya Wateja na Uadilifu wa Soko

Tanzania, kupitia Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kushirikiana na Shirika la Viwango Zanzibar (ZBS), limepata fursa ya kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa 72 na Vikao vya Baraza la Shirika la Kanda la Viwango Afrika (ARSO), vitakavyofanyika kuanzia tarehe 23 hadi 28 Juni 2025 huko Zanzibar. Tukio hili la heshima linawaleta pamoja wadau wakuu, viongozi wa sekta mbalimbali na watoa maamuzi kutoka kote barani Afrika kujadili na kuelekeza mustakabali wa viwango barani Afrika.

Katika tukio hili, TBS wamewaalika wadau mbalimbali pamoja na kampuni mshirika wake wa kibiashara – SICPA Tanzania – kuonesha dhamira yao ya pamoja katika kukuza ukuaji wa viwanda, biashara na ulinzi wa watumiaji, pamoja na kuonyesha maendeleo ya Serikali ya Tanzania katika kulinda mapato ya kodi na kuhakikisha viwango na ubora wa bidhaa.

SICPA Tanzania inashirikiana na TBS katika lengo la kuendeleza viwango, usalama na ufuatiliaji kupitia teknolojia bunifu na ya kisasa. Ikiwa na wafanyakazi zaidi ya 150 nchini ambao ni raia wa Kitanzania, SICPA Tanzania inashirikiana na TBS katika utekelezaji wa Mfumo wa Uhakika wa Mafuta (Fuel Integrity Solution) kuhakikisha ubora wa mafuta, kulinda mapato ya kodi na kupunguza udanganyifu. Kampuni pia inasaidia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kufikia malengo yake ya ukusanyaji wa mapato, kuimarisha utii wa sekta binafsi na kupambana na biashara haramu kupitia Mfumo wa Stempu za Kielektroniki (ETS).

Kama kiongozi katika teknolojia, SICPA na suluhu zake za uthibitisho zinawawezesha serikali kulinda bidhaa zinazopaswa kufuata viwango maalum vya ubora na usalama, kutambua bidhaa bandia na zisizo na viwango, kuongeza uelewa wa watumiaji, na kujenga imani ya watumiaji kwa viwango na alama za serikali. Pia huchangia kupunguza ushindani usio wa haki, kuongeza ushindani kwa wazalishaji na waingizaji halali, kuboresha usimamizi na utekelezaji wa mamlaka za mitaa katika soko, na kuhakikisha usalama na uhalisia wa bidhaa kupitia ufuatiliaji wa mnyororo wa usambazaji.

“Tunajivunia kushirikiana na TBS katika ARSO 2025 na kuwasilisha suluhisho za SICPA Tanzania kwa ofisi zote za viwango Afrika, mbele ya Makamu wa Rais wa pili wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, pamoja na viongozi na wadau wa ngazi ya juu wa kanda katika masuala ya viwango. Tunaheshimika kwa kusaidia mamlaka kufikia malengo yao makubwa na kuwalinda pamoja na kuwawezesha watumiaji wa Tanzania kupitia ubunifu wa kisasa wa usalama na ufuatiliaji wa bidhaa,” alisema Bw. Alfred Mapunda, Mkurugenzi Mkuu wa SICPA Tanzania.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...