.jpg)
*AJIRA MILIONI 1 BARANI AFRIKA MNAMO 2024 – RIPOTI YAONESHA
KATIKA masoko ya nchi 54 Barani Afrika, Kampuni ya Coca‑Cola na kampuni za rasmi za kuuza bidhaa zake (bottlers), ambao kwa pamoja wanafahamika kama mfumo wa wa Coca-Cola, walichangia TSH 27.04 trilioni ($10.4 billion) katika uchumi mnamo 2024.
Mfumo wa Coca‑Cola uliwezesha zaidi ya ajira 1 milioni katika biashara rejareja, kilimo, viwanda, uchukuzi na huduma Barani Afrika.
Mfumowa Coca‑Cola ulitumia TZSH11.44 trilioni ($4.3 bilioni) Barani Afrika mnamo 2024, kiasi ambacho ni sawa na 83% fedha zilizotumiwa katika manunuzi ya bidhaa na huduma Barani Afrika.
[Johannesburg, Afrika Kusini] (23 June 2025) – Kampuni ya Coca-Cola imetangaza matokeo ya utafiti wa kina kuhusu mchango wake katika ustawi wa kiuchumi na kijamii barani Afrika, wakati wa Mkutano wa Biashara kati ya Marekani na Afrika wa mwaka 2025 uliofanyika Luanda, Angola.
Mfumo wa Coca-Cola uliwezesha zaidi ya ajira milioni moja katika mlolongo wake wa thamani barani Afrika katika sekta kama vile rejareja, kilimo, uzalishaji wa viwandani, usafirishaji na huduma. Hii ni pamoja na ajira 36,800 za moja kwa moja ndani ya mfumo wa Coca-Cola, pamoja na ajira zisizo za moja kwa moja zipatazo 987,000 zinazoungwa mkono katika mlolongo huo. Hii ina maana kuwa kwa kila kazi moja ya moja kwa moja, mfumo huu uliwezesha ajira nyingine 27.
Utafiti huo, uliofanywa na kampuni ya kimataifa ya ushauri wa kitaalamu ya Steward Redqueen, unaonesha kuwa mfumo wa Coca-Cola uliwekeza dola bilioni 4.3 za Kimarekani katika uchumi wa Afrika mwaka 2024 kupitia ununuzi wa bidhaa na huduma kutoka kwa wasambazaji wa ndani ya Afrika, kiasi kinachowakilisha asilimia 83 ya manunuzi yake yote.
“Uwepo wetu wa muda mrefu barani Afrika, tukishirikiana na wasambazaji na wauzaji wa ndani, umetuwezesha kuendeleza ukuaji endelevu na kuchangia maendeleo ya bara hili,” alisema Luisa Ortega, Rais wa Kitengo cha Uendeshaji cha Afrika katika Kampuni ya Coca-Cola.
“Mfumo wetu wa kipekee wa uendeshaji hutuwezesha kuleta athari chanya za muda mrefu katika jamii tunazofanyia kazi.”
Mifuko ya bidhaa za kampuni hiyo barani Afrika inajumuisha bidhaa mbalimbali katika aina tofauti ya vinywaji. Viambato na vifungashio vinavyotumiwa na mfumo wa Coca-Cola barani Afrika hupatikana kwa kiasi kikubwa ndani ya nchi, na huzalishwa, kutengenezwa na kusambazwa kwa ushirikiano na wazalishaji wa ndani.
“Ahadi ya Kampuni ya Coca-Cola kwa Afrika bado ni thabiti,” Ortega alisema.
“Mfumo wa Coca-Cola umetangaza uwekezaji wa karibu dola bilioni 1.2 za Kimarekani barani Afrika katika kipindi cha miaka mitano ijayo, na tunatumaini kuwa mazingira thabiti na yanayotabirika ya sera yatawezesha uwekezaji zaidi katika miezi na miaka ijayo. Aidha, mfumo wa Coca-Cola utawekeza takriban dola milioni 25 kufikia mwaka 2030 kusaidia kushughulikia changamoto muhimu zinazohusiana na maji katika jamii za mitaa katika masoko 20 ya Afrika.”
Utafiti huu unaangazia nafasi ya mfumo wa Coca-Cola katika ukuaji wa muda mrefu wa Afrika na katika kuendeleza maendeleo endelevu kote barani. Mbinu iliyotumiwa na Steward Redqueen inachanganya takwimu za kiutendaji zilizotolewa na wateja na vyanzo vya kuaminika vya uchumi na viwango vya tasnia. Mbali na kupima mchango wa moja kwa moja pekee, uchambuzi huo unaonesha uhusiano wa kiuchumi, unaoonesha jinsi mfumo wa Coca-Cola unavyochochea uzalishaji, kutengeneza kipato na kusaidia ajira katika sekta mbalimbali na maeneo tofauti.
Teodora Nenova, Mshirika Msimamizi katika Steward Redqueen, aliongeza: “Tathmini yetu ya athari inaonesha ukubwa wa mchango wa kiuchumi wa mfumo wa Coca-Cola barani Afrika. Matokeo haya yanaangazia ukubwa wa uwepo wa Coca-Cola katika maeneo ya ndani na mchango wake endelevu katika fursa za kiuchumi na riziki kote barani.”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...