TAASISI ya Mtetezi wa Mama, imetoa Rai kwa Watanzania kuwa na moyo wa upendo na mshikamano kwa kushiriki katika shughuli zinazolenga kusaidia makundi yenye mahitaji maalumu katika jamii kwa lengo ili kuunga mkono dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Kauli hiyo imetolewa leo Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Neema Karume ikiwa ni siku moja baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwaasa wananchi kudumisha mitazamo chanya kuhusu watoto wenye changamoto mbalimbali za kiafya.
Akizungumza hatua hiyo, Neema amesema Rais Samia akiwa ndiye Mama Kiongozi katika Taifa, ana kila sababu ya kuungwa mkono kwa juhudi mbalimbali anazozionesha kukemea Imani potofu zinazochangia watoto hao kufichwa au kutengwa katika jamii.
Awali akizungumza juzi wakati wa kilele Cha Harambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo Cha kulelea watoto wenye Mahitaji Maalumu cha Bagamoyo, iliyoandaliwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Rais Samia Suluhu Hassan alisema watoto wenye ulemavu hawapaswi kufichwa wala kutengwa, bali wapewe fursa sawa ya malezi, elimu na ustawi kama watoto wengine.
" Rais wetu ni mtu mwenye upendo wa hali ya juu sana, amekuwa akipigania ustawi wa makundi yote akiwa kama Mama, nasi kwa nafasi yetu kama Taasisi ya Mtetezi wa Mama tulioamua kuwa mstari wa mbele kuunga mkono mambo anayoyasimamia tunawasisitiza wananchi kumuunga mkono" alisema Neema
Alisema kwa kufanya hivyo kimsingi kutasaidia kuendelea kumpa moyo wa kuendelea kuwatumikia wananchi wake kwa juhudi, upendo na maarifa na hivyo kuliwezesha Taifa kufikia malengo yake ya kujiletea maendeleo na umoja miongoni wa watu wake.
Neema amesisitiza kuwa tangu Rais Samia aingie madarakani, ameonesha uwezo mkubwa wa kiuongozi jambo lililomuwezesha kutunukiwa tuzo mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania hatua iliyomfanya kujizolea sifa nyingi kutoka kwa makundi mbalimbali.
Kadhalika, ameongeza kuwa Taasisi ya Mtetezi wa Mama, imekuwa na zaidi itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wanaounga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Samia katika kuliletea maendeleo Taifa hili la Tanzania analoliongoza huku akiwataka watanzania kuwaepuka watu wanaotaka kuivuruga amani iliyopo.
Amesema Mtetezi wa Mama yanye wanachama wake nchi nzima, ipo bega kwa bega na na watu wote wanaopenda Amani huku wakikuomba Mungu amjalie afya njema Kiongozi huyo ili aendelee kuwatumikia watanzania wote.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...