
Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetunukiwa tuzo ya hadhi ya juu kwa mara ya sita mfululizo iitwayo European Quality Choice Diamond ya mwaka 2025 katika hafla iliyofanyika usiku wa tarehe 29 Mei, 2025, jijini Stockholm, nchini Uswidi, kwa kutambua utendaji wake mahiri katika utalii na uhifadhi.
Tuzo hiyo ilikabidhiwa na Mshauri Mtendaji Mkuu wa taasisi ya European Society for Quality Research (ESQR), Bw. Michael Harris, kwa Balozi wa Tanzania nchini Uswidi, Mhe. Mobhare Matinyi, ambaye aliambatana na Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, Bw. Mussa Nassoro Kuji; Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Rodwell Ole Meing'ataki; Afisa Mkuu wa Uhifadhi, Eunice Msangi; Afisa Uhifadhi Andrew Mbai; na Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania, Malik Hassan.
TANAPA ilikuwa kampuni pekee ya utalii na uhifadhi kati ya 49 kutoka nchi 42 duniani zikiwemo zingine sita za Afrika iliyotunukiwa tuzo hiyo. TANAPA ni moja ya taasisi kadhaa nchini zenye usajili wa ISO 9001:2015 ambacho ndicho kigezo cha kupimwa utendaji na ESQR kila mwaka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...