Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amekutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Wang Yi pembezoni mwa Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano baina ya China na Afrika (FOCAC) jijini Changsha, China tarehe 10 Juni, 2025.
Katika mazungumzo, Mhe. Wang Yi ameeleza kwamba China itachukua hatua kuendeleza kwa vitendo uhusiano mzuri na wa kihistoria uliopo baina ya Tanzania na China ambao uliasisiwa na waasisi wa mataifa hayo mawili, Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania na Mao Zedong wa China ikiwemo kutekeleza kwa wakati mradi wa kuikarabati reli ya uhuru (TAZARA), ambao ni kielelezo cha ushirikiano imara kati ya China na Afrika.
Mhe. Wang Yi vilevile ameahidi ushirikiano wa Serikali ya China katika ufadhili na utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati nchini Tanzania kwa ajili ya kuongeza kasi ya maendeleo.
Mhe. Waziri Kombo ametumia nafasi hiyo kuishukuru Serikali ya China kwa namna ambavyo imekuwa ikiunga mkono jitihada za maendeleo za Serikali ya Tanzania kwenye nyanja mbalimbali.
Akiwasilisha vipaumbele vya nchi katika utekekezaji wa maeneo 10 ya ushirikiiano yaliyotangazwa na China, Mhe. Waziri Kombo ameeleza kwamba katika utekelezaji wa mpango kazi wa Jukwaa la Ushirikiano wa Kiuchumi Kati ya China na Afrika (FOCAC), Tanzania itaweka kipaumbele kwenye miradi ya miundombinu, maendeleo ya kilimo, viwanda na rasilimali watu.
Kwa mahsusi ameomba Serikali ya China kurahisisha taratibu zake kwa ajili ya kuongeza nafasi kwa bidhaa za Tanzania kulifikia soko hilo.
Kadhalika, wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika masuala ya kimataifa yenye maslahi kwa pande zote mbili. Hii ni sehemu ya jitihada za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki za kuendelea kutekeleza Sera ya Mambo ya Nje yenye msisitizo katika Diplomasia ya Uchumi katika kutangaza fursa mbalimbali ikiwemo biashara, uwekezaji na utalii.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...