NA. MWANDISHI WETU – GENEVA USWISI
Tanzania yaendelea kung’aa Kimataifa katika kukinadi Kituo cha Ufuatiliaji wa Mwenendo wa Majanga na Tahadhari ya Mapema (National Emergency Operation and Communication Center Situation Room) katika Kituo cha Taifa cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura nchini Tanzania ambacho kimeifanya nchi kuwa kinara katika masuala ya menejimenti ya maafa hususan katika kuzuia, kupunguza kujiandaa na kukabili maafa pindi yanapotokea.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi ametoa kauli hiyo tarehe 03 Juni, 2025 Mjini Geneva nchini Uswisi wakati alipohudhuria Jukwaa la Nane la Dunia la Nnae la Kupunguza Madhara ya Maafa ili kutathmini, kujadili maendeleo ya utekelezaji wake na kuimarisha masuala ya usimamizi wa maafa kimataifa kupitia makubaliano ya hiyari ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ambayo yameridhiwa linaloendelea Mjini humo.

Akizungumzia masuala ya menejimenti ya maafa amesema Tanzania imenufaika kwa uwepo wa kituo hicho ambapo,kimeendelea kutumika kufanya ufuatiliaji wa uwezekano wa kutokea kwa majanga kwa kutumia mifumo ya kiteknolojia ya kijiografia kwa majanga yanayotokana na hali ya hewa na haidrolojia kwa kutumia jukwaa la kielektroniki la MyDEWETRA.

Aidha aliongezea kuwa Tanzania inajiandaa kuwa Kituo cha Kikanda kwa ajili ya wadau mbalimbali kujifunza namna ya kukabiliana na majanga katika mazingira ya Afrika na Nchi zinazoendelea hususan Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Dkt. Yonazi ametumia Jukwaa hilo kuyaalika Mataifa kuja kujionea na kujifunza namna Kituo cha Ufuatiliaji wa Mwenendo wa Majanga na Tahadhari ya Mapema kinavyotumika kurahisisha ufuatiliaji wa mwenendo wa janga lililotabiriwa na kufanya uchambuzi wa kiwango cha madhara kwa jamii, miundombinu na mazingira, kuandaa taarifa za tahadhari ya mapema ya hatua za kuchukua za mzingo wa menejimenti ya maafa.

“Tanzania imeweza kushirikisha uzoefu wake katika masuala ya menejimenti ya maafa katika mkutano huo, na tumepata fursa ya kueleza fursa zilizopo nchini, na wenzetu wapo tayari kujifunza kutoka kwetu na namna tunavyokiendesha kituo na wapo tayari kushirikiana nasi,” alisema Dkt. Yonazi

Akiyataja baadhi ya manufaa ya kituo hicho amesema kimeendelea kimendelea kuipa nchi heshima kwa kuwa na mfumo huo unaosaidia katika kukabiliana na pindi yanapotokea.

Naye Mwakilishi Mkaazi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (SRSG) wa Kupunguza athari za Maafa, na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupunguza athari za Maafa (UNDRR),Bw. Kamal Kishore akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi ameipongeza Tanzania namna inavyoendelea kupiga hatua katika masuala ya usimamizi wa Maafa huku akiipigia mfano ikiwa ni moja kati ya Taifa linalotekeleza na kuendelea kufanya vizuri katika kukabiliana na maafa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...