Na Mwandishi Wetu, Mwanza
MAKAMU Mwwnyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amewaeleza wabunge na madiwani hususan waliokuwa wanajifungia vioo kwenye magari wajue wakati umefika.
Amesema uchaguzi mkuu sio ajali na kwamba wabunge na madiwani wanajua kila baada ya miaka mitano hufanyika uchaguzi mkuu huku akieleza wanaotaka kugombea ubunge ni vema wakapima uwezo wao kama ambavyo unapaswa kupima kina cha maji kwa fimbo kabla ya kuvuka mto kusombwa na maji.
Wasira ameyasema hayo leo Juni 23, 2025, alipokuwa akizungumza na viongozi wa CCM kujiandaa kwenda kutiki ifikapo Oktoba na kwa nafasi ya urais tayari Chama kimepitisha jina la Dk. Samia Suluhu Hassan na mgombea mwenza ni Dk. Emanuel Nchimbi.
“Kwa upande wa urais tumemaliza tumeshaweka mgombea wetu Dk.Samia Suluhu Hassan na kazi yetu ni kumuuza kwa wananchama na wananchi .Kwa wabunge kama ubunge unaisha Juni 27 ndio maana hauwapi presha maana tangu walipoingia walijua ikifika miaka mitano uchaguzi unafanyika.
“Kwa hiyo uchaguzi sio ajali... kama wewe unauogopa labda hukufanya maandalizi maana wako watu katika jamii hata wale waliowachagua hawawajui wale ndio wenye kupata presha... sasa kama unafunga vioo unawapita watu usilaumu watu,” amesema Wasira.
Aidha amesema ubunge unapatikana kwa kujenga mahusiano mazuri na wananchi hivyo ukiwa na mahusiano mazuri na mambo yako(mgombea) yatakuwa mazuri.
Pia amesema uchaguzi umefika na wanachama wana haki ya kuchukua fomu ila alishauri kwa wale wanachama wapya wanaotaka ubunge wakapima nguvu ya waliopo au waliomaliza muda wao.
“Wakati sisi zamani tukiwa watoto ukitaka kuvuka mto maana madaraja hayakuwepo na mito kama inatiririka hivi unaenda na fimbo, unatanguliza fimbo uone kama fimbo itatikiswa na maji, ikitikiswa na maji mpaka take kwenda huingii pale maana utaenda wewe,

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...