Na Mwandishi Wetu

Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi Conrad Milinga amesema, maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yamewezesha Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) kutoa elimu juu ya fursa mbalimbali za kiuchumi kupitia mikopo na mifuko ambayo iko katika sekta mbalimbali zinazohusiana na uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Mkurugenzi Milinga ametoa kauli hiyo leo Juni, 23,2025 wakati wa kilele cha Maadhimisho Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika katika viwanja vya Chinangali park Jijini Dodoma.

Ameeleza, Ofisi ya waziri Mkuu imetumia maadhimisho ya wiki hiyo kueleza wananchi na wadau mbalimbali kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Ofisi hiyo ikiwemo Uwezeshaji wananchi kiuchumi, namba ya kujikinga na maafa na Alama za Taifa ambazo ni Wimbo wa Taifa, Ngao ya Taifa na Bendera ya Taifa.

“Tumeweza kuelimisha wananchi kuhusu mfumo unaotumiwa na Idara ya Menejimenti ya Maafa unaoweza kutambua majanga mapema kabla hayajatokea ili kuwapa wananchi tahadhari ya kujiandaa kabla hayo majanga hayajatokea, tumetoa uelewa kwa wananchi kuweza kufahamu maatumizi sahihi ya Alama za Taifa ikiwemo Ngao sahihi ya Taifa , Beti za wimbo wa Taifa ambapo wimbo huo unatakiwa kuimbwa beti zote mbili na rangi sahihi za Bendera ya Taifa”, amebainisha Milinga

Aidha, ameongeza kuwa, Ofisi imeweza kutoa elimu kwa umma kuhusu Idara ya Ufutiliaji na Tathimini ya shughuli za Serikali inavyohusika katika kutoa taarifa za utekelezaji wa miradi mabalimbali inayotekelezwa hapa nchini.

Mbali na hayo, Mkurugenzi Milinga ametoa wito kwa wananchi kujitokeza katika Maonesho ya Kimataifa ya Sababa ambapo Ofisi ya Waziri Mkuu itashiriki maonesho hayo yanayotarajiwa kuanza tarehe 28 Juni, 2025 Jijini Dar Es Salaam.

“Katika maonesho hayo Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na taasisi zetu zote itanatarajia kushiriki hivyo niwasihi wananchi kutembelea maonesho hayo ili kuweza kupata elimu kuhusu shughuli zote zinazofanya na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Madhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yalianza tarehe 16 Juni, 2025 mpaka tarehe 23 Juni, 2025 chini ya kauli mbiu isemayo “Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidigiti ili Kuongeza Upatikanaji wa Taarifa na Kuchagiza Uwajibikaji”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...