Na Mwaandishi Wetu Mtwara

VIJANA waliojiriwa kupitia programu ya kilimo ya Jenga Kesho Iliyobora (BBT) kama maafisa ugani Mkoani Mtwara wameeleza mkakati wao wa kufanikisha lengo la serikali kuzalisha korosho tani 700,000 mwaka 2025/2026.

Maafisa hao waliajiri na Bodi ya Korosho Nchini (CBT) kupitia programu ya BBT ili kutoa huduma za kilimo, elimu na mbinu za kisasa kwa wakulima wa korosho ili kuongeza tija kwenye zao la korosho nchini.

"Kutokana na mafunzo ambayo tunapewa ninaweza kumhudumia mkulima ,kumpa elimu na mbinu za kuhudumia mikorosho, ajue namna na wakati sahihi wa kuhudumia mfano kupulizia dawa ili kuondoa visumbufu kama magonjwa kwenye mikorosho," amesema Neema Christopher.

Naye Methew Kisum afisa ugani Wilaya ya Masasi chini ya BBT amesema "Tunapenda kuihakikishia serikali kuwa tutafanikisha lengo la kuzalisha korosho kama yalivyo matarajio Yao, tumefundishwa mbinu ,elimu na namna bora kabisa kuhudumia mkulima ili azalisha kwa tija."

Maafisa hao walikuwa wakizungumza wakati wakipatiwa mafunzo na CBT, na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Nchini (TARI) kituo Cha Naliendele Mkoani Mtwara.

Afisa Kilimo Mwandamizi kutoka CBT Geoffrey Mwalembe maafisa hao wanapewa mafunzo ya matumizi sahihi na salama ya kutumia viautilifu vya zao la korosho ili kuwajengea uwezo wa kutoa huduma za kilimo kwa wakulima.

"Mafunzo haya ni moja kati ya malengo ya serikali kupitia Bodi ya Korosho ya kuongeza uzalishaji na tija kwenye zao la korosho kufikia tani 700,000, 2025/2026 na tani 1,000,000 mwaka 20230," amesema.

Serikali kupitia CBT imetoa shilling bilioni 8 kutekeleza Programu ya BBT kwenye kupitia zao la korosho.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...