Farida Mangue, Morogoro
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) imewataka watoa huduma wa tiketi mtandao kuunganisha mifumo yao na mfumo wa serikali inayosimamiwa na LATRA pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kabla ya Julai 1, 2025.
Hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha usimamizi wa sekta ya usafiri ardhini, kuongeza uwazi katika ukusanyaji wa mapato, na kuhakikisha abiria wanapata huduma kwa mujibu wa sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Morogoro wakati wa ukaguzi wa kawaida wa utekelezaji wa masharti ya leseni za usafirishaji abiria, Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na mawasiliano LATRA Salum Pazzy amesema hadi sasa watoa huduma wachache kati ya 15 waliokamilisha usajili na kuunganisha na mifumo yao na mifumo ya serikali
“Baada ya tarehe 30 Juni mwaka huu , watoa huduma ambao hawajakamilisha kujiunga na mifumo ya serikali hawataruhusiwa kuendelea kutoa huduma. Lengo ni kuhakikisha hakuna mianya ya upotevu wa mapato na abiria wanapata huduma iliyo salama na yenye uwazi,” alisema Pazzy.
Pazzy amewataja watoa huduma hao wa tiketi mtandao ni pamoja na Logix Co Limited, Itule Company Limited, Busbora Company Limited, Duarani Innovate Limited, Web Corporation Tanzania Limited, Hashtech Tanzania Limited, Otapp Agency Company Limited, Sepa Tech Limited,Iyishe Company Ltd - Adventure Connection,Global Light & Company Limited, Mkombozi Infotech Company Limitedl, Meerkatz - Kidia One, Abood Bus Services, Borita Company Limited na Exabytes Africa Ltd.
Pazzy amesema LATRA kwa kushirikiana na jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani. wanaendelea na ukaguzi wa mabasi ya abiria kote nchini, Ukaguzi huo unahusisha ufuatiliaji wa uhalali wa leseni za usafirishaji, Matumizi ya mikanda ya usalama, Uwekaji wa alama kwenye mizigo ya abiria na Uzingatiaji wa matumizi ya tiketi mtandao.
Aidha, LATRA imeonya kuwa wahudumu wa mabasi ambao hawajasajiliwa na mamlaka hiyo hawatoruhisiwa kuendelea kutoa huduma, hatua zitachukuliwa dhidi ya wasafirishaji wanaokiuka matakwa hayo.
“Wahudumu wote lazima wawe wamepata mafunzo kutoka Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) pamoja na chuo cha Taifa cha usafirishaji (NIT), wawe na vitambulisho rasmi, na watoe huduma kwa kuzingatia nidhamu, usafi, na staha kwa abiria.”
Kwa mujibu wa LATRA, baadhi ya makosa yanayorudiwa mara kwa mara na wahudumu ni pamoja na kuweka muziki usiofaa, kuruhusu biashara holela ndani ya mabasi, na kushindwa kudhibiti mizigo ya abiria.
Kwa upande wao baadhi ya wahudumu wa mabasi wamepongeza hatua inayochuliwa na LATRA ya ukaguzi wa mabasi kwani unawakumbusha wajibu wao katika kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa abiri wakati wote wa safari.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...