CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema hakitaahirisha uchaguzi ng'o kwa sababu kiliomba ridhaa ya kuongoza nchi kwa miaka mitano na kimeongoza vizuri kwa kuleta maendeleo chini ya serikali iliyoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan

Hayo yameelezwa leo Juni 9,2025 na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira alipokuwa akiwasalimia wanachama, wapenzi wa Chama na wananchi waliofika ofisi za CCM Mkoa wa Ruvuma kumlaki akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo.

"Tuliomba ridhaa ya kuongoza Tanzania kwa miaka mitano, tumeiongoza Tanzania, tumefanya kazi yetu vizuri halafu unatuambia tuahirishe, ahirisha wewe mambo yako sisi hatuwezi ng'o, sisi tunagombea, tumeshaweka wagombea, tumemuweka Daktari Samia Suluhu Hassan (mgombea urais kupitia CCM), tumemuweka Dk. Emmanuel Nchimbi (Mgombea Mwenza wa CCM).

"Sasa wako rafiki zangu wale wa 'tone tone' wao wanapita wanawaambia tusifanye uchaguzi na mimi nawauliza tukiacha kufanya uchaguzi nchi itakuwa inaongozwa na nani, maana huwezi kuwaambia watu acheni uchaguzi halafu huwapi mbadala eti tuahirishe, tuahirishe nini?," alieleza na kuhoji.

Alisema kuwa kote ambako wamepita na hata ambako bado hawajapita, CCM iko imara na inamuunga mkono Dk. Samia Suluhu Hassan na hawamuungi kwa sababu zozote ambazo hazielezeki, bali wanamuunga kwa sababu ya maendeleo makubwa aliyoyafanya "haya mnayoyasikia ameyafanya Songea ndiyo hayo hayo ameyafanya Tanzania nzima."




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...