Tunduru-Ruvuma.
Jumla ya tani 1,273.487 za ufuta zenye thamani ya Shilingi 3,107,049,390 zimeuzwa katika mnada wa kwanza wa zao hilo uliofanyika katika kijiji cha Mchesi kupitia Chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) cha Mruji, Tarafa ya Lukumbule, Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma.
Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika Wilaya ya Tunduru, Marcelino Mrope, bei ya chini katika mnada huo ilikuwa Shilingi 2,410 kwa kilo, bei ya juu Sh.2,460, huku bei ya wastani ikiwa Sh.2,439.
Alibainisha kuwa, ufuta wote uliokusanywa kupitia vyama vya msingi vya ushirika uliuzwa, japokuwa bei imepungua ikilinganishwa na msimu wa mwaka 2023/2024 ambapo bei ya juu ilikuwa Sh.3,783, ya chini Sh.3,705 na wastani Sh.3,744 kwa kilo moja.
Akizungumza na wakulima wakati wa mnada huo, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Simon Chacha aliishukuru Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa kuweka mazingira mazuri ya kilimo na usimamizi wa masoko, hali iliyowezesha wakulima kunufaika na mazao yao. Aidha, alisisitiza kuwa Serikali ya Wilaya itaendelea kusimamia mfumo wa stakabadhi ghalani kwa kuwa unaleta tija kwa wakulima.
Pia aliwahimiza wakulima kutumia taasisi za kifedha kupokea malipo yao ili kuepuka usumbufu na ucheleweshaji wa malipo. Alitoa wito kwa wakulima kutumia vizuri mapato yao kwa kuboresha maisha, kujenga nyumba bora na kusomesha watoto badala ya kuzitumia kwenye matumizi yasiyo ya lazima.
Akigusia upatikanaji wa pembejeo, Chacha alisema Serikali tayari imeanza kugawa pembejeo za sulphur kwa ajili ya kupulizia korosho, na kuonya kuwa ni marufuku kwa yeyote kuuza pembejeo hizo zilizotolewa kwa ruzuku. Alisisitiza kuwa wakulima wanapaswa kununua pembejeo kwenye maduka rasmi yanayouza kwa bei iliyopunguzwa kulingana na mwongozo wa Serikali.
Kwa upande wake, Kaimu Afisa Kilimo wa Wilaya ya Tunduru, Gallus Makwisa, aliwapongeza wakulima kwa kuvuka lengo la uzalishaji wa ufuta kutoka tani 4,000 msimu wa kilimo 2023 hadi kufikia tani 8,000 msimu wa 2024. Alieleza kuwa Halmashauri kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa imesambaza tani 8,000 za mbegu bora za ufuta katika kata 36 za wilaya hiyo ili kuongeza uzalishaji na ubora wa zao hilo.
Makwisa aliwataka wakulima kuzingatia usafi na ubora wa ufuta kwa kusafisha maghala na kuhakikisha mazao yao hayachanganywi na uchafu kabla ya kuuzwa sokoni, ili kuendelea kushindana kwenye soko la ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wake, Afisa Masoko wa TAMCU, Stella Msengi, alisema kuwa katika msimu wa kilimo wa mwaka 2024/2025, jumla ya kilo 8,774,621 za ufuta zilikusanywa na kuuzwa – ikiwa ni ongezeko la kilo 4,800,997 sawa na asilimia 60.09 ikilinganishwa na msimu uliopita. Bei ya wastani msimu huo ilikuwa Sh.3,684.54 kwa kilo.
Aliongeza kuwa kwa msimu wa 2025/2026, malengo ni kukusanya kilo 12,811,100 za ufuta, sawa na ongezeko la asilimia 46. Alihimiza wakulima kuendelea kushirikiana na vyama vya msingi vya ushirika kwa ajili ya kuuza mazao yao kupitia mfumo wa mnada unaoleta uwazi na manufaa kwa mkulima.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...