Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila akizungumza wakati akifungua kikao Kazi kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wa Manispaa ya Ubungo na Kinondoni kilichoandaliwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO )jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Lazaro Twange akitoa maelezo kuhusiana na kikao kazi ya Tanesco na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wa Manispaa ya Ubungo na Kinondoni  kilichofanyika jijini Dar es Salaam.


*Ataka kazi yao ionekane waachane na dili

Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam,Albert Chalamila amesema kuwa wenyeviti wa serikali ya mtaa wanawajibu wa kulinda miundombinu ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ili shirika hilo liendelee kutoa huduma kwa wananchi.

Amesema kuwa haiwezekani watu wanaharibu miundombinu ya Tanesco ikiwemo wa wizi mafuta kwenye Trasfoma huku mwenyekiti wa mtaa yupo hivyo inaonyesha hakuna uwajibikaji na kuongeza kuwa wapo wenyeviti wanafatilia 'dili' kwa ajili ya kujipatia rushwa na kuacha miundombinu ya Tanesco ikiharibika ndani ya mtaa wao.

Chalamila aliyasema hayo wakati akifungua kikao kazi kati ya Tanesco na Wenyeviti wa Serikali ya Mitaa wa Manispaa ya Ubungo na Kinondoni ikiwa ni Kampeni ya Tanesco ya Lipa Deni ,Linda Miundombinu Tukuhudumie kilichifanyika katika Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.

Amesema wenyeviti wa Serikali za mitaa ni wadau muhimu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Serikali kwa kuwa miradi hiyo hutekelezwa katika maeneo yao ya kiutawala hata miradi mingi ya TANESCO iko kwenye mitaa yao.

"Ni imani yangu kuwa kupitia kikao kazi hiki wenyeviti wote wanakwenda kuwa mabalozi wa kueleza huduma nzuri zinazotolewa na TANESCO pia kulinda miundombinu ya Shirika hilo” Amesema RC Chalamila.

Aidha ameipongeza TANESCO kwa kuona umuhimu wa kukutana na kundi hilo muhimu ili liweze kufahamu kwa kina majukumu ya shirika hilo lakini pia kutoa mawazo na ushauri wa namna bora ya kuboresha utoaji wa huduma za nishati ya umeme kwa wananchi hususani katika mitaa yao.

RC Chalamila amepongeza TANESCO kwa kuandaa kikao na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya ya Kinondoni na Ubungo kwa kuwa ni wadau muhimu.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Lazaro Twange amesema Shirika hilo kwa kutambua Wenyeviti wa Serikali za mitaa ni wadau muhimu likaona liandae kikao kazi kwa ajili yao ili kutengeneza mfumo mzuri wa mawasiliano ambao utatusaidia kujua wananchi wanasemaje kuhusu huduma za TANESCO pia wenyeviti wawe na uwezo wa kuelewa nini kinafanywa na shirika pamoja na kuwaelimisha wananchi walioko katika maeneo yao.

Asema utekelezaji wa miradi ya TANESCO uko kwenye ngazi ya mitaa ambayo huongozwa na wenyeviti wa Serikali za Mitaa.

Mhandisi Twange amesema kuwa kikao hicho ni muhimu sana kutokana na kutambua wenyeviti hao kwenda kuwa msaada baada ya kikao hicho.

Amesema Serikali inatumia fedha nyingi katika miundombinu hivyo miundombinu hiyo inatakiwa kulindwa na wenyeviti wa Serikali ya Mtaa ndio sehemu kubwa miradi hiyo iko kwao.

Katika Kikao hicho Mkuu wa Mkoa Chalamila amemkabidhi majiko ya kupikia kwa umeme viongozi hao ambayo yanatumia umeme kidogo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan za kuhamasisha matumizi ya Nishati safi kwa Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...