Mgeni rasmi wa NBC Dodoma Marathon 2025, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Tsh. milioni 100 Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Amref Tanzania Dkt. Florence Temu (wa pili kushoto) iliyotolewa na Benki ya NBC kwa kwa Ajili ya kufadhili mafunzo kwa wauguzi 100 ili kusaidia watoto wenye changamoto ya usonji kupitia mbio za NBC Dodoma Marathon 2025 zilizofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw. Theobald Sabi (wa pili kulia) na viongozi wengine kutoka serikalini na wadau wa mbio hizo.

Mkurugenzi Mkazi wa Amref Tanzania, Dr. Florence Temu akiambatana na viongozi mbalimbali wakati wa NBC Dodoma Marathon 2025, 27/07/2025, Dodoma.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Amref Tanzania wakati wa mbio za NBC Dodoma Marathon 2025, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma 27/07/2025.

Mkurugenzi wa Miradi Amref Tanzania, Dkt. Aisa Muya (Wa pili kushoto) akiambatana na viongozi mbalimbali wakati wa NBC Dodoma Marathon 2025, 27/07/2025, Dodoma.
*

Dodoma, Tanzania, 27 Julai 2025 – Amref Health Africa – Tanzania imepokea msaada wa shilingi milioni 100 za Kitanzania (sawa na takribani dola 38,500 za Kimarekani) kutoka Benki ya NBC wakati wa mbio za NBC Marathon 2025 zilizofanyika Dodoma. Fedha hizo zitatumika kufadhili mafunzo kwa wauguzi 100 ili kusaidia watoto wenye changamoto ya usonji.


Mbio hizo, zilizowakutanisha mamia ya washiriki kutoka sehemu mbalimbali za nchi, hazikuwa tu jukwaa la kuhamasisha afya ya mwili, bali pia fursa ya kuendeleza athari chanya za kijamii na huduma jumuishi za afya.


NBC Marathon 2025 iliyofanyika Dodoma ililenga kuimarisha mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi, kuboresha afya ya mama na mtoto, na kufadhili mafunzo kwa wauguzi 100 ili kusaidia watoto wenye changamoto ya usonji.


Mchango wa shilingi milioni 100 za Kitanzania (sawa na dola 38,500) utawezesha Amref Tanzania kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya wa ngazi ya msingi kuhusu utambuzi, usimamizi, na utoaji wa huduma kwa watoto wenye changamoto ya usonji.


Jitihada hizi zinaendana na dhamira ya Amref Tanzania ya kuhakikisha huduma bora, jumuishi na zinazozingatia mahitaji ya jamii zinapatikana kote nchini.


Akizungumza katika tukio hilo, Dkt. Florence Temu, Mkurugenzi Mkazi wa Amref Tanzania, alitoa shukrani za dhati kwa ushirikiano wa NBC na dhamira yao ya kusaidia kuboresha huduma za afya.


“Msaada huu kutoka NBC ni hatua muhimu katika jitihada zetu za kuboresha huduma kwa watoto wenye changamoto ya usonji hapa Tanzania. Mafunzo kwa wahudumu wa afya ni msingi muhimu kwa utambuzi wa mapema na utoaji wa huduma jumuishi kwa watoto wenye changamoto hii,” amesema Dkt. Temu.


“Tunapongeza NBC kwa uwekezaji wake endelevu katika afya na ustawi wa jamii zetu.”


Mchango wa NBC unaonesha dhamira yake ya kweli ya kuwajibika kwa jamii na kuboresha maisha ya makundi yaliyo katika mazingira magumu kupitia ushirikiano wa kimkakati.


Amref Tanzania inaendelea kushirikiana na taasisi za serikali, asasi za kiraia na sekta binafsi katika kujenga mifumo ya afya inayojumuisha kila mtu, hususan wale wanaoishi na usonji na changamoto nyingine za kimaendeleo.


Baadhi ya Watumishi wa Amref Tanzania wameshiriki mbio za marathon zijulikanazo kama NBC Dodoma Marathon 2025.




Matukio katika picha wakati wa mbio za NBC Dodoma Marathon 2025, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma 27/07/2025.
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...