Kassim Nyaki, NCAA.


Kamishna wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Abdul-razaq Badru amewataka askari wa uhifadhi wa taasisi hiyo kuendelea kulinda rasilimali za wanyamapori, Misitu na malikale kwa ari na weledi ili taifa liendelee kunufaika na rasilimali hizo.

Kamishna Badru ametoa maelekezo hiyo katika kilele cha siku ya askari wanyamapori duniani (World Rangers Day) leo tarehe 31 Julai, 2025 ambapo mamlaka hiyo imedhimisha siku hiyo katika viwanja vya mnadani Karatu Mkoani Arusha.

Amesema mamlaka inatambua mchango wa askari wa uhifadhi kutokana na kujitoa kwao kulinda rasilimali hizo hivyo iko tayari kuboresha utendaji wao ili uendane na mabadiliko ya sayansi na teknolojia. Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kutambua mchango huo imewapa vyeti na fedha kufuatia juhudi na kujitoa kwao katika ulinzi wa kupambana na vitendo vya ujangili hali iliyosaidia kuokoa rasilimali za wanyamapori, mali za shirika na askari wengine.

“Maadhimisho haya ni maalum kwa ajili ya kutambua na kuenzi mchango wa askari wanyamapori wanaolinda hifadhi na rasilimali zilizopo, Tanzania ikiwa miongoni mwa mataifa yenye urithi mkubwa wa bioanuai, inao wajibu wa kuwaenzi askari wa uhifadhi ambao ni mashujaa wetu wa ulinzi wa wanyamapori na misitu kwa maslahi ya nchi yetu na vizazi vijavyo”alisema Kamishna Badru.

Akielezea maadhimisho ya siku hiyo Kaimu Meneja Idara ya Huduma za Ulinzi Mhifadhi Mwandamizi Linus Tiotem ameeleza kuwa tangu kuanzishwa kwa Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro jumla ya askari 11 wamepoteza maisha kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ujangili, ujambazi na kuuawa na wanyamaopri.

Siku ya Askari wa Wanyamapori Duniani ilianza kuadhimishwa mwaka 2007 kwa lengo la kuwakumbuka askari waliopoteza maisha wakati wa kutekeleza majukumu yao, kauli mbiu ya maashimisho ya mwaka huu ni “ Rangers: Powering Transformative Conservation” ikilenga kuutambua mchango wa askari wa Wanyamapori katika kuleta mabadiliko ya kweli katika uhifadhi wa maliasili ambayo ni urithi wa Taifa.












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...