Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo Julai 24,2025

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, ametembelea kiwanda cha kuunganisha magari aina ya FAW cha Rostar Vehicle Equipment Ltd ,wilayani Bagamoyo na ameridhishwa na kazi kubwa inayoendelea kufanyika . 

Amepongeza wawekezaji hao kushirikisha vijana wa Kitanzania kupata ajira na mafunzo ya kuunganisha magari hayo.

"Vijana wana uwezo! Ni wabunifu, wachapakazi na wenye ,” alisema  Kunenge . "

Mkurugenzi wa kiwanda, Bai Xinguo, alieleza ,kiwanda hicho cha kuunganisha magari ya FAW ni kikubwa Barani Afrika. 

"Kiwanda hiki kinatarajia kuunganisha hadi magari 500,000 kwa mwaka na tayari kimepokea oda ya magari 1,000 kutoka kwa wateja mbalimbali. Pia kitaproduce trailers, matanki (tanks) na cranes."

Hata hivyo, aliomba Serikali kusaidia kuboresha barabara ya kufika kiwandani ambapo mkuu wa mkoa alhaj Kunenge aliahidi kushughulikia suala hilo kwa kushirikiana na mamlaka husika.

Vilevile Kunenge alimuagiza ,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo kuanza upangaji wa mji na kuhakikisha wamiliki wa ardhi wanafuata ramani ya mipangomiji.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...