-Asema Serikali sikivu ya Rais Dkt Samia Suluhu imesikia kilio hicho mwarobaini tayari umepatikana.
Mku wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila amefanya ziara katika Kituo cha mabasi yaendayo haraka DART kilichopo Kimara mwisho Wilaya ya Ubungo na kuitaka mamlaka inayosimamia mabasi yaendayo haraka UDART kuboresha huduma zao ili kumaliza adha wanayopitia wananchi wanaotumia usafiri huo.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo RC Chalamila amesema hajaridhishwa na huduma hiyo ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka kutokana na uchache wa mabasi jambo ambalo limekua likichangia huduma mbovu na kuwasababishia watumiaji wa usafiri huo adha kubwa kinyume na dhamira ya Rais Dkt Samia ya kutaka kuboresha huduma yq usafiri katika Jiji hilo,hivyo ameitaka UDART kuboreha huduma.
Aidha RC Chalamila ametembelea upanuzi wa barabara ya Ubungo Kimara unaosimamiwa na TANROAD ambapo ameitaka mamlaka hiyo kumsimamia mkandarasi amalize ujenzi huo kwa wakati pia ameshauri uwepo wa huduma za vyoo kwenye maeneo ya vituo vikubwa ikiwemo kimara.
Kwa upande wake Menaja upangaji ratiba na udhibiti kutoka UDART Daniel Madilu amesema tayari wameshafanya tathmini ya changamoto ya usafiri huo na kwamba tayari wameagiza mabasi miamoja kutoka China yatakayoingia nchini mwezi wa tisa mwaka huu
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila ametembelea mamlaka ya kusimamia ujenzi wa barabara za mwendokasi DART iliyopo Ubungo maji jijini humo na kueleza mikakati ya Serikali chini ya Rais Dokta Samia kumaliza changamoto ya usafiri wa mwendokasi ambapo kwa mradi wa kimara wamepata mwekezaji mpya anaitwa Trans Dar wakati kwa barabara ya Mbagala wamepata mwekezaji anaitwa Mophat wanaotarajia kuingiza magari yao hivi karibuni
Vilevile Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa DART Dkt Othman Kiamia ameahidi kushughulikia changamoto zilizopo kwa sasa ili kuondoa kero kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kusimamia uingizaji mabasi yakutosha na yenye ubora kukidhi uhitaji wa huduma hiyo ya usafiri wa mwendokasi

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...