Wizara ya Maliasili na Utalii imepongezwa kwa kutekeleza kikamilifu maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwa Wizara ya kwanza kukamilisha ujenzi wa jengo la Ofisi na kuwezesha Idara na Vitengo vyake kuhamia Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma.

Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. William Lukuvi alipotembelea Wizara hiyo kwa lengo la kukagua ujenzi wa Majengo ya Serikali ambao ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu ya Serikali kuhamia Dodoma.

Mhe. Lukuvi amesema kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii licha ya kukamilisha mapema ujenzi wa jengo hilo, inastahili pia kupongezwa kuwa wa kwanza kuhamia na kuwa mfano katika Matumizi ya samani za Ofisini zilizozalishwa hapa nchini kupitia mazao ya Misitu.

"Ninyi ni mabalozi wazuri wa Matumizi ya bidhaa zetu za hapa nchini zinazotokana na Misitu yetu, niimani yangu kuwa Wizara zote zitaiga mfano huu". Aliongeza Mhe. Lukuvi

Aidha Mhe. Lukuvi ametoa rai kwa watumishi wa Wizara hiyo kuhakikisha wanatunza vyema miundombinu na vifaa vilivyopo ili viweze kudumu kama ilivyo kusudiwa.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi amemshukuru Waziri Lukuvi kwa ziara yake, na kuahidi kuwa Wizara itatekeleza vyema maelekezo aliyoyatoa hususani ya usimamizi mzuri wa Matumizi ya jengo na vifaa vilivyopo.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...