Wito huo umetolewa na Mratibu wa Mkoa wa Mafunzo Ndg. Tumaini Ng'unga kwa Niaba ya Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe.Magdalena Rwebangira wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa Watendaji ngazi ya Jimbo ambapo amewasisitiza kuwa endapo watakiuka viapo hivyo watakuwa wamevunja sheria na watawajibika kwa kutenda kosa hilo.

Aidha Ndg. Ng'unga amewataka Watendaji hao kuhakikisha wanajiridhisha na taarifa kabla ya kuzitoa kwenye vyombo vya Habari na kuipima taarifa wanayotaka kuitoa ili kuepuka kuleta taharuki katika jamii.

"Washiriki wa mafunzo katika utekelezaji wa majukumu yenu mnapaswa kutoa taarifa mbalimbali kwenye vyombo vya Habari ili kuwajulisha wananchi na wadau mambo mbalimbali ya uchaguzi, Sasa nitumie fursa hii kuwasihi kwamba iwapo kutakuwa na uhitaji wa kutoa taarifa jiridhisheni kwanza na ikiwezekana washirikisheni wenzenu...kabla ya kutoa taarifa...ili kuepuka kuleta taharuki" Ameeleza Ndg. Ng'unga

Mafunzo haya yenye lengo la kuwajengea uwezo watendaji wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo kutoka mikoa ya Rukwa na Katavi yamemalizika leo tarehe 23 Julai, 2025.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...