Na Diana Byera,Bukoba


Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Taifa imerejesha jina la Mhandisi wa TANROAD Mkoa wa Kagera, Johnstoni Mtasingwa, ambaye anakaimu Kitengo cha Mipango na ni msimamizi wa Kitengo cha Mizani Kagera, huku akichuana na wenzake wanne katika kumpata mwakilishi mmoja wa kupeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Bukoba Mjini.

Mtasingwa, ambaye ana mchango mkubwa katika usimamizi wa miradi ya miundombinu ya ujenzi wa barabara na madaraja, amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na usimamizi wake wa Daraja la Kitengule linalounganisha kiwanda cha Kagera Sukari katika Wilaya ya Missenyi na Karagwe.

Usimamizi wa Barabara ya Kyamihorwa Buzirayombo yenye urefu wa kilometa 120, pamoja na kusimamia uwekaji wa taa za barabarani Bukoba Mjini na usanifu wa ujenzi wa Daraja la Mto Kanoni na njia za mji wa Bukoba.

Amesema dhamira yake ni kuleta mabadiliko katika masuala ya miundombinu bora na huduma zinazogusa maisha ya watu, uongozi shirikishi kuanzia ngazi ya shina hadi ngazi ya mkoa.

Kujenga uelewa kwa vikundi vya wanawake na vijana ili waweze kunufaika na asilimia 30 inayotengwa katika bajeti ya miundombinu kwa ajili ya kupata ajira za muda na endelevu, pamoja na kuwa na kanzi data ya vijana waliyoitimu na kozi zao ili kuwasaidia kuwaunganisha na fursa za ajira.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...