“Serikali kupitia Mradi wa BOOST imeleta mapinduzi makubwa ya elimu kwetu. Tunashukuru kwa kutujengea madarasa, matundu ya vyoo na kuweka mazingira bora ya kujifunza,” alisema Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mzizima ya Mchepuo wa Kiingereza, Maua Rashid Kibendu, akifungua ziara ya waandishi wa habari shuleni hapo jijini Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo, wanafunzi wa darasa la sita waliwaonyesha wageni umahiri wao wa kuelewa na kueleza masomo ya sayansi kwa Kiingereza. Mwanafunzi Abiero Odwar aliwaelekeza wenzake kwa ufasaha kuhusu mfumo wa hewa na chakula mwilini, huku Subra Saad Kumbata akieleza kwa umahiri njia za uzalishaji wa umeme kwa kutumia vifaa mbalimbali.

Uwezo huo wa wanafunzi unatokana na uwekezaji wa Serikali kupitia Mradi wa Kuimarisha na Kuboresha Elimu ya Awali na Msingi (BOOST), ambao mwaka 2024 ulitoa zaidi ya shilingi milioni 306 kwa ajili ya uanzishwaji wa shule hiyo.

Kupitia fedha hizo, shule imepata madarasa tisa, matundu 16 ya vyoo, na miundombinu mingine muhimu, hali iliyoongeza hamasa ya walimu kufundisha na wanafunzi kujifunza. Shule hiyo sasa ina wanafunzi 647 — wavulana 313 na wasichana 334 — na imekuwa kivutio cha wanafunzi kutoka shule nyingine kutokana na ufaulu wa juu katika mitihani ya kitaifa.












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...