Dodoma, 16 Julai, 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-

(i) Bw. Omari Juma Mkangama ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Ludewa;

(ii) Bw. Juma Abdallah Njeru ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mpanda;

(iii) Bi. Hellen Emmanuel Mwambeta ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha;

(iv) Bw. Francis Genes Kafuku ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu;

(v) Dkt. Adam Omar Karia ameteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo cha Maji kwa kipindi cha pili;

(vi) Balozi Dkt. Aziz Ponary Mlima ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi (TISEZA);

(vii) Jenerali Mstaafu Venance Salvatory Mabeyo ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kwa kipindi cha pili.

(viii) Dkt. Harrison George Mwakyembe ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kwa kipindi cha pili;

(ix) Bw. Filbert Michael Mponzi ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Sukari Tanzania kwa kipindi cha pili; na

(x) Dkt. Leonada Raphael Mwagike ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) kwa kipindi cha pili.

Sharifa B. Nyanga
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...