
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Prof. Erick Komba amesema taasisi hiyo ipo tayari muda wote kushirikiana na wafugaji na wadau mbalimbali wa mifugo katika kubaini na kutatua changamoto za mifugo lengo ikiwa ni kuongeza tija kwenye ufugaji kwa kuwa na teknolojia bora na hivyo kuongeza mchango wa sekta ya mifugo kwenye pato la Taifa.
Prof. Komba ameeleza hayo katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. J. K. Nyerere jijini Dar es salaam yakiwa na kauli mbiu isemayo “Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) Fahari ya Tanzania”
“Katika kipindi hiki cha Sababasa tupo katika viwanja hivi kwa ajili ya kutoa elimu na kusambaza teknolojia zetu kwa wafugaji na wadau mbalimbali wa mifugo ikiwemo teknolojia ya malisho na mbegu za malisho, teknolojia ya vyakula vya mifugo, teknolojia ya mbari bora za mifugo” alisema Prof Komba.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa TALIRI Kanda ya Mashariki Dkt. Zabron Nziku amesema ili uweze kuwa na mifugo bora ni lazima kuzingatia kuwa na malisho bora na aina bora ya mbari ya mfugo hivyo TALIRI imekuja na teknolojia bora za mifugo zinazofaa kwa mfugaji wa mifugo yote.
“Katika Maonesho tupo na teknolojia ya boksi ya kufungia majani kwa ajili ya kuyahifadhi vizuri ili yaweze kusaidia kipindi cha kiangazi ambapo majani hayapatikani kwa urahisi” alieleza Dkt. Nziku
Dkt. Nziku ameendelea kueleza kuwa boksi hilo husaidia kutengeneza marobota ‘hay’ kwa njia rahisi na nafuu ambayo mfugaji wa hali yeyote anaweza kumudu, watu wawili wanaweza kutengeneza marobota 350 kwa mwezi na robota moja hutosha kwa ng’ombe wawili kwa siku.
Nae Meneja wa Sehemu ya Uhaulishaji wa Teknolojia wa Taasisi hiyo Bw. Gilbert Msuta amewataka wafugaji na wadau mbalimbali kutembelea banda la TALIRI kwa ajili ya kujipatia elimu ya ufugaji bora na teknolojia bora za mifugo ambazo zitawezesha kuzalisha kwa tajiri









Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...