TANZANIA imeendelea kuonesha uongozi thabiti katika kuimarisha amani, usalama na ushirikiano wa kisiasa katika ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), tangu ilipochukua nafasi ya Uenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (Organ Troika) kuanzia Agosti 2024.
Ameyasema hayo leo Julai 12, 2025 Jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Kombo wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema kuwa chini ya uenyekiti wa Tanzania, mafanikio kadhaa yamepatikana ikiwa ni pamoja na kuandaa mikutano mikubwa ya kikanda, kuongoza misheni za uangalizi wa uchaguzi katika nchi kadhaa, na kushiriki katika juhudi za kurejesha utulivu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
“Tumefanikisha mikutano mitano ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC kujadili masuala ya amani na usalama, kuongoza Mkutano wa Tatu wa Maafisa Waandamizi wa Kamati ya Kisiasa na Kidiplomasia ya SADC, na kuratibu kwa mafanikio mkutano wa kihistoria kati ya SADC na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuhusu usalama mashariki mwa DRC,” amesema Waziri Kombo.
Aidha, amebainisha kuwa Tanzania imechangia vikosi maalum katika operesheni ya kulinda amani ya SADC nchini DRC (SAMI-DRC) na kusimamia urejeo wao kwa mafanikio baada ya muda wao kumalizika.
Kuhusu Mkutano wa 27 wa Kamati ya Mawaziri wa SADC (MCO), Waziri Kombo amesema utazinduliwa rasmi Julai 24–25, 2025 jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo utajadili hali ya usalama katika ukanda huo, mikakati ya kuzuia na kutatua migogoro, pamoja na uimarishaji wa mifumo ya tahadhari ya mapema katika nyanja za kisiasa, kiusalama, kijamii na kiuchumi.
Mkutano huo utafanyika nchini kutokana na nafasi ya Tanzania kama Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, nafasi aliyokabidhiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mnamo Agosti 18, 2024.
Taarifa kutoka Wizara zinaonesha kuwa mkutano huo unatarajiwa kuwahusisha zaidi ya wajumbe 300 kutoka nchi 16 wanachama wa SADC, wakiwemo Mawaziri wa Mambo ya Nje, Ulinzi, Mambo ya Ndani na Usalama pamoja na Maafisa Waandamizi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...