Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), limezitaka mamlaka na taasisi mbalimbali za ujenzi nchini kutumia maaraba za shirika hilo kuangalia ubora wa bidhaa wanazotumia kwenye ujenzi wa miundombinu ili iweze kudumu.
Ameyasema hayo leo Julai 4, 2025, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Dk Ashura Katunzi, wakati ujumbe kutoka Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Maji, Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) na Wakala wa Barabara Nchini (TNROADS) walipotembelea shirika hilo.
Dk Katunzi alisema lengo la ziara hiyo ilikuwa kuangalia uwezo wa maabara ya ujenzi ya shirika hilo na namna bidhaa mbalimbali zinavyopimwa kuhakikisha zinakuwa na ubora unaukubalika.
Alisema TBS ina maabara 12 za kupima bidhaa mbalimbali na maabara zote zimepata ithibati ya kimataifa na zinaweza kutoa majibu yenye uhakika na yanayoweza kutumika kama rejea kwenye maeneo mbaimbali.
Alisema hata wataalamu wanaosimamia maabara hizo wamepata mafunzo ya kimataifa na wameonyesha weledi mkubwa katika kusimamia vipimo mbalimbali vinavyowasilishwa kwenye shirika hilo.
Mhandisi John Malisa kutoka Tanroads, alisema wakala na TBS ni washirika muhimu wa maendeleo kwani ndilo shirika ambalo limekuwa likipima vifaa vyao vinavyotumika kwenye shughuli mbalimbali za ujenzi.
Alisema TBS imekuwa msaada mkubwa kwao katika kuzipa ithibati maabara zao kama zinafanya kazi kwa viwango vinavyokubalika kitaifa na kimataifa.
“Tunashirikiana nao katika kufanya utafiti wa ubora wa ujenzi wa barabara zetu tunafanya usanifu majenzi na kusimamia ujenzi wa baragara kuu na za mikoa sasa ili zidumu muda mrefu na ziwe nzuri lazima suala la ubora lizingatiwe na hapo ndipo TBS anaingia,” alisema
Msajili wa Bodi ya Wahandisi ERB, Benard Kavishe, alisema ziara hiyo imekuwa muhimu kwao kwani wameona namna maabara za shirika hilo zinavyofanyakazi.
Alisema TBS inamchango mkubwa katika sekta ya ujenzi kwani ndiyo imekuwa ikipima ubora wa vifaa vinavyotumika katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali.
Alisema bila kupima vifaa hivyo vya ujenzi kuna uwezekano miundombinu inayojengwa ikawa dhaifu na kuharibika ndani ya muda mrefu baada ya kujengwa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...