Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), jaji Jacobs Mwambegele akizungumza na wawakilishi wa watu wenye ulemavu kutoka asasi mbalimbali nchini katika mkutano wa kutoa elimu na kupokea hoja za kundi hilo kuelekea kwenye uchaguzi mkuu 2025 Jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji (Rufani), Mhe. Jacobs Mwambegele akizungumza katika Mkutano wa Tume na Wawakilishi wa Watu wenye Ulemavu, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, leo Julai 31,2025
Wawakilishi wa Watu wenye Ulemavu wakiwa katika Mkutano wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na wawakilishi hao, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam leo Julai 31, 2025.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji (Rufani), Jacobs Mwambegele (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhani Kailima, wakati wa Mkutano wa Tume na Wawakilishi wa Watu wenye Ulemavu, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), jaji Jacobs Mwambegele (mwenye suti nyeusi waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wawakilishi wa watu wenye ulemavu kutoka asasi mbalimbali nchini katika mkutano wa kutoa elimu na kupokea hoja za kundi hilo kuelekea kwenye uchaguzi mkuu, kulia kwake ni Mkurugenzi wa Tume, Ramadhani Kailima na kushoto kwake ni Kamishna wa Tume, Zakia Abubakary.

Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
WATU wenye ulemavu wametakiwa kuwa mabalozi wa amani na kushiriki kikamilifu katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa kuhakikisha wanawahamasisha wenzao kujitokeza kupiga kura pamoja na kulinda utulivu wa taifa katika kipindi chote cha uchaguzi.
Wito huo umetolewa leo Julai 31, 2025 na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele wakati akifungua mkutano wa Tume na watu wenye ulemavu kuhusu maandalizi ya Uchaguzi Mkuu, uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Jaji Mwambegele amesema kuwa katika kipindi cha kampeni, mara nyingi hushuhudiwa joto la kisiasa kutokana na baadhi ya wananchi kukosa uvumilivu wa kisiasa hali ambayo inaweza kuhatarisha amani na utulivu 2a nchi.
“Kupitia majukwaa yenu, mna nafasi ya kuwa sehemu ya walinzi wa amani...,tunawasihi kuwaelimisha wenzenu wenye ulemavu kuwa makini na kuhakikisha kuwa hawawi chanzo cha kuvuruga amani na utulivu wa nchi yetu katika kipindi cha kampeni,” amesema Jaji Mwambegele
Amebainisha kuwa Tume inatambua mchango na ushiriki wa watu wenye ulemavu katika mchakato wa uchaguzi na ndiyo maana imeandaa kikao hicho mahsusi kwa ajili ya kutoa taarifa na kupokea maoni yao kuhusu maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Aidha, ameeleza kuwa Tume tayari imetangaza ratiba rasmi ya uchaguzi ambapo utoaji wa fomu za urais utaanza Agosti 9 hadi 27, 2025, na uteuzi wa wagombea wote kufanyika tarehe 27 Agosti, 2025. Kampeni zitaanza Agosti 28 na kuhitimishwa Oktoba 28, 2025 kwa upande wa Tanzania Bara na Oktoba 27, 2025 kwa upande wa Zanzibar.
Kwa upande wa ushiriki wa walemavu, Jaji Mwambegele amesema kuwa Tume imekuwa ikijitahidi kuhakikisha mchakato mzima wa uchaguzi unakuwa shirikishi kwa watu wote, ikiwemo wenye ulemavu, kwa kuwapatia taarifa kwa wakati na kuhakikisha mazingira rafiki ya kupigia kura.
Akizungumzia kuhusu elimu ya mpiga kura, alifafanua kuwa hadi sasa jumla ya taasisi 164 zimesajiliwa kutoa elimu hiyo, huku zingine 88 (76 za ndani na 12 za kimataifa) zikiwa zimesajiliwa kwa ajili ya uangalizi wa uchaguzi. Alisisitiza kuwa Tume inatarajia ushiriki mkubwa wa walemavu katika kuwaelimisha wenzao na kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi.
“Tume itafanya kazi kwa karibu nanyi ili kuhakikisha elimu ya mpiga kura inawafikia walemavu wote na kwamba wanajua haki yao, wajibu wao na namna ya kushiriki kikamilifu kwenye zoezi la uchaguzi,” alisema.
Ametoa rai kwa watu wenye ulemavu waliopata vibali vya kutoa elimu ya mpiga kura kuhakikisha wanazingatia sheria, kanuni na maelekezo yote ya Tume katika utekelezaji wa majukumu yao.
Akihitimisha hotuba yake, Jaji Mwambegelege amesema kuwa Tume itaendelea kusimamia uchaguzi kwa kuzingatia Katiba, sheria, kanuni na taratibu ili kuhakikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 unakuwa huru, wa haki, wa wazi na wa kuaminika.
“Kauli mbiu yetu inasema ‘Kura Yako Haki Yako, Jitokeze Kupiga Kura’. Tume inatambua na kuthamini nafasi yenu na itaendelea kuwashirikisha katika hatua zote za mchakato huu,” amehitimisha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...