Wanafunzi katika Shule ya Msingi Azimio iliyopo Halmashauri ya Mji wa Makambako mkoani Njombe, wamefurahia ujenzi wa miundombinu bora na jumuishi inayotoa fursa ya elimu kwa wanafunzi wenye mahitaji Maalum.

Hawa Njovi, mwanafunzi mwenye ulemavu wa viungo mwenye malengo ya kuwa daktari wa watoto, amesema miundombinu rafiki inahamasisha ujifunzaji hivyo amewashauri watoto wasikate tamaa.

Brian Bundala Mwanafunzi katika Shule hiyo amesema madarasa ya zamani hayakuwa salama, lakini miundombinu mipya inawapa hali ya kujiamini zaidi wawapo shuleni.

Naye, Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu Maisha Mhapa ameeleza kuwa BOOST imewezesha ujenzi wa madarasa 9, ikiwemo madara mawili ya Elimu ya Awali, matunda ya vyoo 18 Kwa gharama ya Sh. Milioni 347.5

Afisa Elimu wa Kata ya Mwembetogwa, Esther Njabili ameishukuru Serikali kwa kutekeleza program hiyo kwa mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuwajea uwezo walimu katika stadi mbalimbali.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...