
Wataalamu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA),Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Wizara ya Uchukuzi ,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi pamoja na Halmshauri ya Wilaya ya Kilwa.
*TASAC yajiandaa katika kutoa mafunzo mbalimbali mara baada ya kuanza bandari hiyo
Na Mwandishi Wetu ,Kilwa
WATAALAM wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA),Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Wizara ya Uchukuzi ,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi pamoja na Halmshauri ya Wilaya ya Kilwa wameunda kamati ndogo ya kutafuta mbinu bora ya uendeshaji wa Bandari ya Uvuvi Kilwa mara baada ya kukamilika.
Kikao hicho kimefanyika baada ya ujenzi Bandari hiyo kufikia asilimia 82 ili mara baada ya kukamilika uende sambamba na uendeshaji.
Akizungumza katika ziara iliyoandaliwa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) ya kutembelea Bandari ya Kilwa , Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi Wizara ya Uchukuzi Biseko Chiganga amesema timu hiyo ya wataalamu ikikamilisha kazi yake itatoa muelekeo ya namna ya uendeshaji wa bandari na kupeleka ngazi za juu.
Biseko amesema timu hiyo ya wataalamu, imejumuisha wataalamu katika kuwa na mipango ya kufanya Bandari hiyo kusimamia katika viwango vya Kimataifa katika uendeshaji wa Bandari ya Uvuvi.
"Tumefanya ziara katika mradi na kufanya kikao cha pamoja kuangalia kabla ya mradi kukamilika tuangalie changamoto zilizopo na namna ya kuendesha bandari hii kwa ngazi ya wataalamu, kwani yapo mambo ya kitaalamu kwa ngazi ya awali, hizi kamati za kitaalamu zikikamilisha kazi yake ndio utatoa mwelekeo wa uendeshaji wa bandari,"amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Udhibiti na Usimamizi wa Huduma za Usafiri Majini Nelson Mlali amesema wametembelea kujionea ujenzi wa bandari hiyo ili kujipanga namna ya uendeshaji wake mradi utakapokamilika.
"Sisi TASAC ni wadhibiti wa usafiri wa njia ya maji tumewaeleza wadau na majukumu yetu mradi utakapokamilika, mradi huu ukikamilika unakuwa bandari na bandari na bandari ni moja ya wadau unaodhibiti huduma zake kwa hiyo tumeeleza namna ambavyo tutaisimamia bandari hii,"amesema Mlali
Mlali amesema miongoni mwa majukumu yao bandari hiyo ikikamilika ni kuwapa elimu mabaharia watakaoendesha huduma za meli za uvuvi,usimamizi wa mawakala wa meli,forodha pamoja na kampuni ndogo ndogo za kusimamia huduma za vyakula.
Akizungumzia manufaa ya mradi huo, Jackson Ally mkazi wa Kilwa Masoko amesema vijana watakuza uchumi kutokana shughuli zitazokuwepo katika Bandari hiyo.
"Bandari hii kwetu tunaiona kama faraja yetu, mazao ya uvuvi yataongezeka kwasababu uvuvi utakuwa wa kisasa,tutapata ajira na vijana wengi wataondoka vijiweni na kuchangamkia fursa "amesema.
Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi Wizara ya Uchukuzi Biseko Chiganga akizungumza na waandishi kuhusiana ziara ya kutembelea mradi huo namna utavyoendeshwa kitaalam kwa viwango vya kimataifa vya uendeshaji wa bandari ya uvuvi nchini.
Mkurugenzi Udhibiti na Usimamizi wa Huduma za Usafiri Majini Nelson Mlali akizungumza kuhusiana na TASAC katika shughuli zitazofanyika mara baada ya Bandari ya Uvuvi itapoanza kufanya kazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...