Dar es Salaam, 26 Agosti 2025

Kampuni inayoongoza barani Afrika katika huduma za usafiri kwa njia ya mtandaoni, Bolt Tanzania, imemtangaza Juju Kida kuwa mshindi wa kwanza wa shindano lake la Bolt TZ Dance Challenge, lililofanyika kuanzia Julai hadi tarehe 25 Agosti.

Shindano hili lililojumuisha muziki, ngoma na tamaduni, limevutia mamia ya washiriki kutoka maeneo mbalimbali nchini, likidhihirisha ubunifu na ari ya vijana wa Kitanzania.

Kampeni hii iliendeshwa kupitia wimbo wa asili uitwao “Safari ni Bolt”, uliotungwa mahsusi kuonesha roho ya harakati na mshikamano.

Wataalamu maarufu wa uchezaji Angel Nyigu na Dogo Noma waliongoza shindano kwa kutoa miondoko ya mwanzo, ambayo washiriki waliiga na kuiboresha kwa mitindo yao binafsi.

Juju Kida, ambaye awali alishinda TSh 300,000 katika shindano la ngoma lililoandaliwa na kampuni ya michezo ya kubashiri, ameibuka kidedea kwa umahiri wake wa kisanaa na ubunifu wa kitamaduni.

Kwa ushindi huu, amejinyakulia Tsh 2.5M, heshima ya kitaifa na nafasi ya kutambulika kama moja ya nyota wapya wa dansi nchini Tanzania.Kwa mujibu wa kampuni hiyo, kampeni hii ilikuwa juhudi ya kuungana kwa dhati na kwa uhalisia na jumuiya zake pana za wakazi na abiria.

Peace Watiri, Meneja Masoko wa Bolt Kanda ya Afrika Mashariki, alianzisha mpango huu kwa lengo la pia kutoa jukwaa kwa vijana wanaocheza dansi kuonesha vipaji vyao mbele ya umma.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi tuzo, Dimmy Kanyankole, Meneja Mkuu wa Bolt Tanzania na Kenya, alisema:

“Ngoma ni zaidi ya burudani—ni lugha ya kitamaduni. Shindano hili linaonesha dhamira ya Bolt katika kusaidia vipaji vya ndani huku tukijipambanua kama zaidi ya huduma ya usafiri mtandaoni:

Sisi ni sehemu ya safari, nyakati na mitindo ya maisha ya kila siku.”Bolt Tanzania inaendelea kubuni mbinu mpya za kushirikiana na jamii, ikichanganya teknolojia na utamaduni ili kuwawezesha na kusherehekea vipaji vya Kitanzania.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...