Mafunzo yanayotolewa katika vyuo vya VETA yanalenga kuleta utatuzi wa changamoto mbalimbali katika jamii.
Watu wengi wanaoshi maeneo ya mijini wamekuwa na maeneo finyu kwa ajili ya kilimo, hali hiyo ikampelekea Mwalimu Gema Ngoo wa Chuo cha VETA Kihonda, kubuni bustani ya mbogamboga inayohamishika.
Akizungumza leo, tarehe 5 Agasti ,2025 katika Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo (Nanenane), yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma Mwalimu Ngoo ambaye anafundisha Fani ya Ufundi wa Zana za Kilimo amesema ubunifu huo wa bustani inayohamishika ni mahkususi kwa wale watu wanaoishi katika nyumba za kupanga, nyumba zenye maeneo finyu au zilizosakafiwa kote, hivyo kupelekea kukosa sehemu ya kupanda mbogamboga.
“Ubunifu huu utawasaidia wengi wenye maeneo finyu kwaajili ya kupanda mbogamboga, tunashauri watu walime kilimo cha aina hii kwani hakiharibu mazingira lakinini pia kilimo hiki utatumia mbolea ya asili ambayo ni salama kwa afya za binadamu” amesema Ngoo.
Mwalimu Gema amewaalika wananchi wa Dodoma na mikoa jirani kutembelea banda la VETA lililopo katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma ili kujifunza ubunifu na kupata taarifa za fursa za mafunzo mbalimbali katika vyuo vya VETA.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...