
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA) imeendelea kung'aa katika Maonesho ya 32 ya Kimataifa ya kilimo(NANENANE), 2025 yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
VETA inatumia Maonesho hayo kutangaza fursa za mafunzo ya muda mrefu na mfupi yanayotolewa katika vyuo vyake kote nchini pamoja na kuonesha huduma,vifaa na bunifu zinazotolewa na kutengenezwa na wanafunzi, wahitimu na walimu wake.
Miongoni mwa huduma zinazopatikana kwenye banda la VETA katika maonesho ya Nanenane, 2025 ni pamoja na:
Teknolojia ya uchanganyaji wa vyakula vya mifugo kama vile kuku, samaki na ng'ombe, huduma inayowapa elimu wafugaji juu ya uchanganyaji bora wa vyakula kulingana na uhitaji wa mnyama.
Elimu kuhusu utoaji wa chanjo sahihi kwa mifugo hasusan magonjwa ya mlipuko yasiyokuwa na tiba ikiwepo kideri, kichaa cha mbwa, ndui n.k.
Elimu kuhusu utengenezaji wa mabanda bora na ya kisasa ya kufugia ili kumrahisishia mfugaji kufuga kisasa na kuzalisha mazao yenye tija iliyotolewa na mwalimu Ladslous Chemele wa fani ya Afya ya wanyama na uzalishaji kutoka chuo cha VETA-Singida.
Elimu kuhusu teknolojia ya uchakataji na usindikaji nyama kwa lengo la kumsaidia mfugaji kuondokana na upotevu wa chakula baada ya kuvuna mazao ya nyama (Post harvest losses).
Elimu kuhusu matumizi sahihi ya nyama ili kuepukana na magonjwa yanayoweza kuambukizwa kutoka kwenye nyama/mifugo kwenda kwa wanadamu na mbinu za uhifadhi bora wa zao la nyama ili kutumika wakati wa uhaba.
Elimu kuhusu utunzaji, usalama na Mikato mbalimbali ya nyama na usimamizi wa maduka ya kuuzia nyama iliyotolewa na Mwalimu Veronica Awese kutoka karakana ya Uchakataji na usindikaji nyama ya chuo cha VETA-Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...