Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt Natu Mwamba amewataka washiriki wa Mafunzo na Kikao Kazi cha Mfumo wa CBLS Uliyoboreshwa kuzingatia Ushauri na Maoni yanayoibuliwa katika kikao hicho ili kiwe kikao chenye Tija na Nyenzo muhimu katika kuhakikisha Mipango na Bajeti zinaandaliwa na kutekelezwa kwa kuzingatia Vipaumbele vya Serikali.

Dkt Natu ameyasema hayo leo Jijini Dodoma Agosti 21,2025 kwa washiriki wa Mafunzo ya Mfumo wa CBLS ulioboreshwa na Kikao kazi cha Tathmini ya Utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya mwaka 2024/25 na Maandalizi ya Bajeti ya Serikali ya mwaka 2025/26 pamoja na kupata maoni yatakayoboresha Mipango hiyo.

Na kuongeza kuwa ili kuwa na Kikao chenye tija ni vema kushirikiana kikamilifu katika kikao hicho kwani uzoefu na mawazo hutofautiana,hivyo wakibadilishana mawazo ma uzoefu huo watatoka wakiwa na mipango thabiti na yenye tija.

"Nasisitiza Kuzingatia Ushauri na Maoni yanayoibuliwa wakati wa majadiliano ya kikao kazi hiki ili kikao kazi hiki kiwe chenye tija na nyenzo muhimu katika kuhakikisha mipango na bajeti zetu zinaandaliwa na zinatekelezwa kwa kuzingatia Vipaumbele vya Serikali".

Kwa upande wake Bwana Said Mabie ambaye ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango Ofisi ya Makamu wa Rais amesema kuwa Mafunzo haya yana umuhimu mkubwa kwasababu lengo kubwa ambalo wanalijadili ni kuhakikisha namna gani ambavyo mapato ya nchi yanaweza kusaidia kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo nchini na yale matokeo yanayaotarajiwa kwa Watanzania yanafikiwa kupitia mapato hayo ambayo yanapatikana.

Naye Justin Kisoka ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ameeleza kuwa moja ya mambo yaliyosisitizwa na Katibu Mkuu huyo ni Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050,hivyo Dira hiyo ya 2050 inakwenda kuwa kipimo Chao lakini pia mpango wa miaka 5 sehemu ya 4 lazima uzingatiwe ili kwa pamoja kama Taifa kuweza kufikia malengo yaliyotakiwa kufikiwa kwenye Dira hiyo ya Maendeleo ya Taifa 2050.

Kikao kazi hiki na Mafunzo haya kimewajumuisha Wataalam kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo Wizara,Idara zinazojitegemea,Wakala wa Serikali, Ofisi za Wakuu wa Mikoa,Mamlaka za Serikali za Mitaa,Vyuo Vikuu,Mashirika ya Umma,Wadau wa Maendeleo IMF na Waratibu kutoka Wizara ya Fedha na Tume ya Mipango.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...