-Aitaka NIRC iendelee kufanya kazi kuwafikia wakulima

-Asema utachochea uzalishaji na kukabiliana na ukame




📍NIRC:Dodoma


Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan, amesema katika kufikia azma ya mapinduzi sekta ya kilimo Serikali imechukua hatua ya kufanya uwekezaji mkubwa sekta ya Umwagiliaji lengo likiwa ni kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Amesema, Serikali imeimarisha kilimo cha Umwagiliaji kwa kujenga mabwawa, kukarabati skimu za Umwagiliaji, kuchimba visima katika maeneo yanayokabiliwa na ukame.

Rais Dkt. Samia amesema anataka kuona Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inaendelea kufanya kazi ili kuchochea uzalishaji na huduma zinazotolewa katika sekta ya Umwagiliaji ziwafikie wakulima kuanzia wale wa wadogo, wa kati na wakubwa, lengo likiwa ni kuongeza uzalishaji wa chakula nchini na uzalishaji wa mazao yenye tija

Rais Dkt. Samia amesema hayo wakati alipotembelea eneo la Umwagiliaji wakati wa kufunga Maonesho ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Kitaifa na Kimataifa katika Viwanja vya Nane Nane Nzuguni, jijini Dodoma.

Amesisitiza kuwa kwa mwaka wa fedha 2024/2025 zaidi ya heka 700,000 zimeeendelezwa kwa kuwekewa miundombinu ya Umwagiliji na tayari zinatumika kwa ajili ya kilimo nchini.

“Nilipofika hapa eneo la kwanza kwenda ni kuangalia teknolojia zinazotumika katika kilimo vha Umwagiliaji ningependa wakulima wote waende waone Serikali inavyofanya mambo kwa wakulima,”amesema.

Pia ameongeza “Hadi June mwaka 2025 Wizara ya Kilimo imekamilisha ujenzi wa skimu mpya tatu, ukarabati wa skimu saba na ununuzi wa mitambo mitatu ya kuchimbia mabwawa na mitambo 30 kwa ajili ya uchimbaji wa visima.

Vilevile Serikali imeendelea na utekelezaji wa mirafi 780 nchini yenye jumla ya hekta 543366, ambayo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Miradi hiyo inajumlisha ujenzi wa skimu mpya 63, ukarabati wa skimu 48, ujenzi wa mabwawa 114, ujenzi wa miundombinu katika mambonde 22 ya kimkakati na uanzishaji wa mashamba makubwa sita ya pamoja, upembuzi yakinifu na usanifu 527 unaendelea ambapo kukamilika kwa mirafi hiyo kutaongeza eneo la Umwagiliaji kutoka hekta 727,000 hadi 1,200,000.

Amesema Serikali imefanya mapinduzi makubwa katika sekta ya kilimo cha Umwagiliji nchini na kuitaka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuendelea kufanya makubwa kwa maslahi ya Taifa.

Rais Dkt. Samia ameipongeza Tume kwa hatua kubwa iliyofikiwa katika kuhakikisha Watanzania wanapata huduma za kilimo cha Umwagiliaji kwa uhakika na kusisiza umuhimu wa kuendeleza teknolojia na miundombinu ya Umwagiliaji, ili kuongeza uzalishaji na kuwa na uhakika wa chakula na mazao, hususan katika kipindi cha mabadiliko ya tabianchi.

“Mi nataka Tume ifanye kazi izalishe, mnyororo wote wa Kilimo hadi kufikia kuwa na mazao umekaa vizuri hivyo tuongeze hamasa kwa taasisi, vitengo vyote ikiwemk vya ubora ‘quality yake’ kushirikiana ikiwemo wale wanaozalisha mbegu, wazalishe zaidi, anayehifadhi mazao ahifadhi, anayesimamia Umwagiliaji ajue anafanya nini, anaye ‘ control’kodi ya mazao ajue,”amesema.

Ameongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha hadi kufikia mwaka 2030 sekta ya kilimo Tanzania isimame na kuwa imara kuliko ilivyo sasa.

Aidha ameipongeza Tume kwa hatua kubwa iliyofikiwa katika kuhakikisha Watanzania wanapata huduma za kilimo kwa uhakika, huku akisisitiza umuhimu wa kuendeleza teknolojia na miundombinu ya Umwagiliaji ili kuongeza uzalishaji wa mazao, hususan katika kipindi cha mabadiliko ya tabianchi.

Pia Rais Dkt. Samia amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Tume Raymond Mndolwa kuhakikisha teknolojia zilizopo Tume zinawanufaisha wakulima nchini.

Pia alishuhudia mitambo mbalimbali iliyopo katika maonesho hayo, mashamba ya mfano yanalimwa kwa kutumia maji ya umwagili kwa njia ya mifereji, mipira ya kunyunyiza maji na mazao yanayomwagiliwa kwa njia ya matone na visima vilivyosimikwa mitambo ya umwagiliji.

Akimkaribisha Rais katika eneo hilo, Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ameeleza kuwa mitambo inayooneshwa katika eneo hilo ni mfano wa teknolojia zinazoendelea kuenezwa katika maeneo mbali mbali nchini, kupitia Tume ya Umwagiliaji Bashe ameongeza kuwa Mtambo mkubwa wa umwagiliaji(Centre Pivot) tayari unatumika katika baadhi ya maeneo yakiwepo mashambamba ya serikali yenye ukubwa wa zaidi ya hekta 13,000.

“Mheshimiwa Rais, kama ulivyo elekeza,teknolojia za Umwagiliji unazoona ndiyo teknolojia ambazo tunatumia katika mashamba yote ya mbegu , yanayo milikiwa na serikali”, amesema Bashe.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Tume, Mndolwa amefafanua kuwa Tume imeandaa na kuonesha teknolojia za Umwagiliji zinazotumiwa na wakulima kuanzia wadogo hadi wale wa mashamba makubwa.

“Mheshimiwa Rais, lengo letu kukuleta hapa ni ili uweze kushuhudia teknolojia za kawaida katika umwagiliaji zinazotumkwa na mkulima wa mdogo hadi zile za mashamba makubwa,

“Tume tunakushukuru kwa kutupatia fedha kwa ajili ya ununuzi wa mitambo ya uchimbaji wa visima na kwamba Tume imepokea pia fedha ya ununuzi wa pump na imeshanunua pump 2,000, ambazo zinasambazwa katika maeneo yasiyohitaji uchimbaji wa visima, kama maeneo ya mradi wa Ziwa Tanganyika na Victoria ambapo tutatumia maji kidogo kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira kwa ajili ya Umwagiliaji,”amesema.

Ameongeza kuwa Tume inafanya mazungumzo na Kampuni za PAG na Pro Agro ili kujenga viwanda ya mitambo ya Umwagiliaji nchini lengo ni kuongeza ajira, thamani ya fedha za ndani na kurahisisha upatikanaji wa mitambo hiyo hapa nchini.













Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...