Na Mwandishi wetu, Pololeti Ngorongoro
Kamishna wa Uhifadhi Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Bw. Abdul-razaq Badru amewataka askari wa uhifadhi katika Pori la Akiba la Pololeti Wilayani Ngorongoro kuzingatia maadili, weledi na matokeo ya kazi wanazozifanya ili kulinda hadhi ya jeshi hilo.
Kamishna Badru ametoa rai hiyo alipokuwa katika ziara ya kikazi na kuzungumza na baadhi ya askari hao alipotembelea Pori la Akiba la Pololeti kukagua hali ya uhifadhi na ulinzi katika eneo hilo.
Aidha Kamishna Badru ameridhishwa na kazi kubwa inayofanywa na askari hao hali iliyosababisha eneo hilo kwa sasa kuwa na idadi kubwa ya wanyama mbalimbali wakiwemo tembo, twiga, simba, swala, pofu, nyumbu, pundamilia na spishi nyingine za wanyama.
Badru amewahakikishia askari hao kuwa miundombinu mbalimbali ya eneo hilo itaboreshwa sambamba na kujengewa mazingira bora ya kufanyia kazi ili kuendelea kuboresha mazingira ya ulinzi na uhifadhi endelevu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...