Na John Jayros

Mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) wa Jimbo la Rufiji, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema akichaguliwa tena atashirikiana na wananchi wa jimbo hilo kuboresha uchumi baada ya mapinduzi makubwa yaliyofanyika katika kipindi chake.

Mhe. Mchengerwa ametoa kauli hiyo leo wakati akinadi sera zake katika Mkutano Mkuu wa Wilaya wa kuomba ridhaa ya kuchaguliwa tena na wanachama katika kata za Mbwara, Chumbi na Mohoro.

Aidha, Mhe. Mchengerwa amesema katika kipindi chote cha ubunge wake wa miaka 10 jimboni hapo alibeba fikra za wananchi wa Rufiji jambo ambalo limesaidia kutimiza ndoto za wananchi na maendeleo makubwa yanayoonekana.

Ameyataja baadhi ya mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi hiki kuwa ni pamoja na ujenzi wa shule za kidato cha tano na sita kutoka shule moja hadi saba, shule za kidato cha kwanza hadi nne zilikuwa nne tu na sasa zimefika 23.

Kuhusu Shule za Msingi amesema zilikuwa 20 na sasa zimefikia 63 huku vituo vya afya vikiongezeka toka vitatu hadi tisa.

Pia amesema wakati anaanza ubunge jimbo halikuwa na barabara za ndani za lami lakini sasa lina takribani kilomita 20 na taa za barabarani zaidi ya 200.
"Ukweli ni kwamba Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imefanya kazi kubwa sana kwenye jimbo letu. ni katika kipindi hiki ambapo tumeshuhudia ongezeko la madaraja toka madaraja 3 hadi 7 ambapo daraja la Mohoro peke yake limegharimu bilioni 17". Amefafanua

Akizungumzia mipango mahususi ya kiuchumi itakayosaidia Mhe. Mchengerwa amesema tayari wamejitokeza wawekezaji wa Kilimo cha Migomba, miwa na kiwanda cha mafuta ya mawese, na kusisitiza kuwa uwekezaji huu utazalisha ajira nyingi kwa akina mama na vijana.


Ameongeza kuwa katika kipindi hiki Rufiji imepandishwa haji kuwa Halmashauri ya jiji jambo ambalo litawezesha kupata miradi mbalimbali ya Benki ya Dunia yenye thamani ya bilioni 30.

Pia amefafanua kwamba katika kipindi hiki jimbo limeunganishwa umeme toka asilimia 17 hadi takribani asilimia 100 ya vijiji vyote vya jimbo hilo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...